Spika Ndugai: Uingereza kuna Mbunge aliapishiwa hospitali akiwa amelazwa na "bahati" mbaya alifariki bila kwenda Bungeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,883
141,815
Mfano huu wa Spika Ndugai wa Mbunge wa Uingereza kuapishwa akiwa "mahututi" hospitalini na kwamba alikufa hapo hospitalini bila kukanyaga Bungeni unafikirisha.

Mstaafu Msekwa alisema Spika ni kama daktari anayepokea wagonjwa wengine wanapona na kuondoka na wengine wanakufa na kuondoka.

Kumbe kuapishwa ni jambo moja na kuingia Bungeni ni jambo lingine.

Hii inanikumbusha kuna watu huingia katika sakramenti ya ndoa takatifu wawapo kufani.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!

Maendeleo hayana vyama.
 
Mwaka 1972 Senator Joe Biden (Rais mteule wa USA) aliapishwa akiwa hospitalini akiwauguza watoto wake wawili walionusurika kwenye ajali mbaya ya gari iliyochukua maisha ya mke wake na binti yake mdogo! Suala la wapi mtu anaapishwa linategemea na mazingira kulingana na kanuni zilizopo.
 
No. Maendeleo yana chama. Kwa miaka kadhaa Uturuki ilikuwa ikichukuliwa kama 'mtu mgonjwa wa Ulaya' kutokana na ubovu wa uchumi wake. Vyama kadhaa vimekuja vikaondoka lakini havikuweza kuuguza gonjwa gumu la kufanya uchumi wa Uturuki angalau ufanane hata na ule wa nchi maskini zaidi Ulaya (kabla ya Umoja wa Ulaya) Ureno.

Fast Forward, kimekuja chama cha Adala (Justice) cha Prime Minister Rajab Orduwan....hivi sasa Uturuki ndiyo yenye uchumi imara zaidi Ulaya, kiasi Wazungu (kama kawaida yao) wanaanza kuiweka mizengwe na kuipiga vita.

Uturuki ndiyo yenye fleet kubwa zaidi ya ndege duniani, ina uwanja mkuu zaidi wa ndege duniani, inazalisha vitu viwandani zaidi kuliko nchi zote za Ulaya ukitoa Ujerumani! Nani anasema maendeleo hayana chama? Kitoeni hicho chama chenu kizee muone kama nchi haitapaa!
 
Hawa CCM waje waseme ni vitu gani tuwaige mabeberu na vipi tusiwaige!

Akitoa mfano kama huo mpinzani, unasikia hao mabeberu, mfano ametoa Ndugai wanakuwa akina nani?

Think again. Ukijielimisha juu ya legacy ya mfumo wa Bunge letu, utatambua kuwa huku sio kuiga. Practices za mabunge ya nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Madola zinashahibiana sana!
 
Kwahiyo anawaiga Mabeberu
Neno mabeberu ni neo la siku nyingi sana halikuanza leo. Neno hili liliingizwa katika lugha za siasa mwishoni mwaa miaka sa sitini hasa baada ya nchi nyingi ikiwemo Ujerumani Magharibu kutaka kuibana Tanzania iifukuze Ujerumani ya Mashriki pale Zanzibar, na lilitokana kutokana na tabia ya mbuzi mabeberu wanavyotaka kutawa kundi lote la mbuzi.

Lililetwa lililetwa kama tafsri ya kiswahili ya empirialists. Maneno mengine yalikuwa ukoloni mambo leo, yaani neocolonialism, ubepari yaani capitalism, ukabaila yaanu feudalism, ujima yaani communalism na mengineyo mengi.

Katika kipindi kimojawapo cha baraza la kiswahili RTD mwaka 1990 kuna msemaji mmoja alisema kuwa iwapo Shaaban Robert akiweza kufufuka leo na akasikia kuwa kuna watu duniani hapa wanaitwa mabeberu atashangaa sana.

Kwa hiyo neno mabeberu siyo la leo na wala lisikusumbue, bali ni masamiati umekuwapo nchini kwa zaidi ya miaka 50 sasa.
 
Back
Top Bottom