Spika Ndugai: Tunaomba Rais aitishe kikao cha Wanaume tu

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
3,991
2,000
Spika wa Bunge, Job Ndugai ametaka kuanzishwa kwa dawati la wanaume ambalo litakuwa linashughulikia changamoto wanazokumbana nazo wanaume. Amesema kwa sasa mkazo umekuwa zaidi kwa wanawake, watu wakidhani wanaume wapo salama, jambo ambalo si sahihi.

"Tutamuomba Mhe.Rais siku nyingine aite mkutano wa wanaume tu, na sisi tu-revenge, wanawake waone wakwetu utakavyokuwa mkubwa zaidi ya wa kwao".
 

Manton

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,019
2,000
Sawa kabisa, ubaguzi ni donda ndugu, haliponi, hadi ukatwe mfupa.
 

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
5,460
2,000
Uanaume ni ujasiri, kusimamia misingi sahihi ya haki na sheria, je yeye atapenya kwenye hilo kundi?
 

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
15,838
2,000
20210610_105612.png
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,763
2,000
Ndugai hebu lipa matibabu ya Mh. Lissu, hivi unafikiri hizo hela ni za kwako ? Mbona wewe ulienda india ukajilipa mabillion ya shilling na umma tukabakia kimya? haya madaraka hutakwenda nayo kaburini utayaacha hapa hapa duniani ndugu!! walikuwepo waliojifananisha na Muumba je leo wapo wapi?
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,363
2,000
Na katika huo Mkutano GENTAMYCINE nitanyoosha Mkono na Kumuomba Mheshimiwa Rais Mama Samia awakanye sana wale Wanawake wanaopenda ' Kusagana ' wakiwa wameshakunywa ' Wines ' zao na mkazo mkubwa uwe kwa wale Wanawake wenye Umri wa kuanzia Miaka ya 55 hadi 65 tu ambao ni Wabibi na hawana tu Wajukuu bali sasa wana mpaka Vitukuu na Vilembwe vyao vinakuja.
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
11,913
2,000
Ndugai achana na wanaume tumeumbwa mateso luhangaika acha kudeka deka....
 

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
52,814
2,000
Katika kikao chenu pia iamuliwe wale wanaume ambao ni "ladies and gentlemen" wako upande gani, kama sio wanaume basi muwa send-off waje kambi ya pili.
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,925
2,000
Tumechoka na hii mikutano ya wanawake na nionavyo sasa ni nchi ktk mashindano ya gender. Samia aendelee na wanawake wenzake, wanaume tuendelee na Philip Mpango!

Mkutano wetu hautakuwa na vigelegele, wanamziki na hasa TMK rudini, jiandaeni kuleta burudani.
 

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,445
2,000
Yaani mwaume mzima kama unaogopa mikutano ya wanawake inabidi ujiangalie upya inawezekana una matatizo. Wanawake wanakutana kwasababu ndiyo walezi wa watoto na familia wanaume wa bongo wengi ni kushinda bar, vijiweni, uvivu na kulalamika kila siku. Hii ndiyo sababu Magufuli alipenda kufanya kazi na wanawake
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,661
2,000
Tuna machungu mengi, kweli watuite tu!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
425
500
Yaani mwaume mzima kama unaogopa mikutano ya wanawake inabidi ujiangalie upya inawezekana unamatatizo. Wanawake wanakutana kwansababu ndiyo walezi wa watoto na familia wanaume wa bongo wengi ni kushinda bar, vijiweni, uvivu na kulalamika kila siku. Hii ndiyo sababu Magufuli alipenda kufanya kazi na wanawake
Mwanaume mzima! Una maana kuna cha ziada kwa wanaume, au? Huyu Rais wa kike aliitisha mkutano na wanawake kwa sababu gani? Huyu si anapenda kufanyakazi na wanawake? Unamwambia nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom