Spika Ndugai: Suala la sukari kutolewa ufafanuzi na Waziri wa Kilimo kesho Bungeni

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,352
Spika Job Ndugai amesema kesho Bungeni kutakuwa na uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara ya Kilimo na Waziri wa Wizara hiyo atatolea ufafanuzi suala la kuadimika kwa sukari nchini

Spika Ndugai amewaomba Wabunge kuwa na subira kwani kesho watapata nafasi ya kuchangia na kuzungumzia suala hilo wakati Waziri Japhet Hasunga akiwasilisha hotuba ya Bajeti yake

Spika Ndugai amesema hayo alipokuwa anajibu hoja ya dharura ya Mbunge Ally Saleh, Mbunge wa Malindi aliyekuwa nahitaji ufafanuzi kuhusu kulalamikiwa kwa kupanda kwa bei ya Sukari nchini
 
Africa bana leo tunajadili sukari km nchi while wengine wanajadili vitu vya kimaendeleo na kupambana na covid.

Saivi tuna vitu 2 vinatusumbua
1.covid-19.
2.sukari.

Mungu atupe mwanga naona tunaelekea pabaya sana,Tz ya viwanda inasaka sukari utadhan blue meth.
 
Ha ha ha ha
Africa bana leo tunajadili sukari km nchi while wengine wanajadili vitu vya kimaendeleo na kupambana na covid.

Saivi tuna vitu 2 vinatusumbua
1.covid-19.
2.sukari.

Mungu atupe mwanga naona tunaelekea pabaya sana,Tz ya viwanda inasaka sukari utadhan blue meth.
[/QUOTE
 
Hauhitajiki ufafanuzi, inahitajika SUKARI, a common household ingredient, yaani hitaji la kawaida kabisa la nyumbani...
Mbona wanakuwa hivyi lkn??
Mara ipo bandarini, mara ipo nyingi nchini, ilhali madukani haipo...

Everyday is Saturday.........................:cool:
 
Back
Top Bottom