Spika Ndugai: Siyo lazima mbunge kuapa ndani ya Bunge lililo muhimu ni Mbunge kuapa mbele ya Spika!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,614
141,439
Spika wa bunge la JMT mh Ndugai amesema wananchi wasichanganye kwamba mbunge ni lazima aape akiwa ndani ya bunge, kanuni hazisemi hivyo.

Kwa mujibu wa kanuni kama kuna kikao cha bunge kinachoendelea basi wabunge wapya wataapishwa ndani ya ukumbi wa bunge.

Endapo mbunge atateuliwa wakati bunge halina vikao basi Spika atamwapisha katika sehemu anayoona inafaa na kulijulisha bunge vikao vitakapoanza.

Spika amesema kiapo cha wabunge wa CHADEMA kilichofanyika kwenye viwanja vya bunge ni halali kwa sababu wameapa mbele ya Spika wa bunge na hilo ndio la muhimu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Huu mchezo umechezwa kwaakili kubwa sana. Hata Mbowe anajua mchezo mzima. Ila pia nimeona ni vyema maana hata wakisusa hakuna jipya
Pia Chadema itatumia hao hao wabunge kuleta angalau upinzani kidogo Bungeni na kuifanya CCM ifunguke akili kidogo
 
Kwa kweli maendeleo hayana vyama, ila ufipa wamenuna sana, wanataka kupasuka kwa hasira. Ila naamini kwenye hili hawajakurupuku, pamoja na kuwa inawezekana kulikuwa na ukinzani wa hoja isingekuwa vizuri Mnyika kama KM kuibuka na kukana hadharani, kwa kufanya vile anazidi kuiangamiza chadema kuliko kujenga.

Alitakiwa akae kmy, km hakukubaliana na maamuzi ya wengi angeachia ngazi. Mnyika aachie ngazi, usizidi kuoboa chadema. Mshikamano wa kitaifa niuhimu kuliko maslahi binafsi.
 
Kwa kweli maendeleo hayana vyama, ila ufipa wamenuna sana, wanataka kupasuka kwa hasira. Ila naamini kwenye hili hawajakurupuku, pamoja na kuwa inawezekana kulikuwa na ukinzani wa hoja isingekuwa vizuri Mnyika kama KM kuibuka na kukana hadharani, kwa kufanya vile anazidi kuiangamiza chadema kuliko kujenga. Alitakiwa akae kmy, km hakukubaliana na maamuzi ya wengi angeachia ngazi. Mnyika aachie ngazi, usizidi kuoboa chadema. Mshikamano wa kitaifa niuhimu kuliko maslahi binafsi.
JJ Mnyika atajiunga na CCM hivi karibuni.

Chadema inamilikiwa na Mbowe na Halima Mdee by Mwita Waitara
 
Leo ninyi ndo wa kushabikia kuapishwa wabunge wa chadema??? Kuna nn mnachokifahamu wasichokijua wengine?
 
Nafikiri CDM inapaswa kukubaliana na mazingira ya kisiasa yaliyopo nchini kwa hivi sasa. Huwezi kumsusia nyani shamba la mahindi.

Isipokuwa hata kama kuna misimamo tofauti juu ya ushiriki wa wabunge wa viti maalum bungeni, inawapasa kutafuta mazingira mazuri ya kuweka wazi kwa umma juu ya uungwaji wake mkono ndani ya kikao chao cha kamati kuu. Hapa panaitajika zaidi msimamo wenye busara wa pamoja zaidi ya kuegemea makundi yatokanayo na misimamo ya viongozi wakuu.

CDM inapaswa ijifunze kupitia suala lililowagharimu la kususia vikao vya Bunge la bajeti kwa hoja ya tishio la COVID-19. Licha ya mazingira yenye kushawishi kuhusu uhuni uliofanywa wakati wa uchafuzi mkuu uliopita, bado itawapasa kuwapa nafasi akina mama hawa waliochaguliwa kihalali waweze kupaza sauti zao bungeni ili kukipa chama uwakilishi uliotukuka.

My brother TAL calm down, everyone understand your unquestionable patriotism in this country. There is a lot of leadership potentials in you, time will come to tell and vividly justify this truth.
 
Back
Top Bottom