Spika Ndugai: Siyo lazima mbunge kuapa ndani ya Bunge lililo muhimu ni Mbunge kuapa mbele ya Spika!

Hata kwenye michezo ,' kelele za washangiliaji zikizidi ujue ushindi umekaribia'

Ngoja tuone nani ataibuka bingwa hapa.
 
Hahaha Chadema inayorudisha maendeleo ya taifa leo inalazimishwa kwenda bungeni!.

Kwani wabunge wa ccm hawawezi kuendelea na vikao bila wabunge wa chadema?!

Kama mnajua ccm hawana akili Kwanini mlilazimisha waende bungeni?!
 
Waliofurahi kuapishwa hao wasaliti ni mataga sababu kuu ni wanajua mchezo mzima ! Litakua jambo la ajabu eti ukute harusi ya mwanafamilia inaendeshwa na kufurahiwa na majirani kuliko wanafamilia...
 
Nafikiri CDM inapaswa kukubaliana na mazingira ya kisiasa yaliyopo nchini kwa hivi sasa. Huwezi kumsusia nyani shamba la mahindi.

Isipokuwa hata kama kuna misimamo tofauti juu ya ushiriki wa wabunge wa viti maalum bungeni, inawapasa kutafuta mazingira mazuri ya kuweka wazi kwa umma juu ya uungwaji wake mkono ndani ya kikao chao cha kamati kuu. Hapa panaitajika zaidi msimamo wenye busara wa pamoja zaidi ya kuegemea makundi yatokanayo na misimamo ya viongozi wakuu.

CDM inapaswa ijifunze kupitia suala lililowagharimu la kususia vikao vya Bunge la bajeti kwa hoja ya tishio la COVID-19. Licha ya mazingira yenye kushawishi kuhusu uhuni uliofanywa wakati wa uchafuzi mkuu uliopita, bado itawapasa kuwapa nafasi akina mama hawa waliochaguliwa kihalali waweze kupaza sauti zao bungeni ili kukipa chama uwakilishi uliotukuka.

My brother TAL calm down, everyone understand your unquestionable patriotism in this country. There is a lot of leadership potentials in you, time will come to tell and vividly justify this truth.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
This is the most important thing that everyone of us should take into account!! Naamini hawa wamama watafanya upinzani thabit na kwa kuwa ni wanawake basi tutegemee kuvuta hisia kwenye bunge hili ambalo hali kua na meno angalau jino moja limeongezeka. Wabunge hawa sio wachache wakiwa na uzalendo uliotukuka wataamusha bunge bubu kuwa bunge semi!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom