Katika kuchangia bandiko la Mwalla lililohusu Rais kuteua tume itakayomtangaza yeye kuwa Rais niligusia dhana ya nguvu za bunge, kwa kuuliza "...nieleze jinsi ambavyo Spika anavyoweza kufurukuta...". Nilisema kuwa wote hao wanaoitwa wakuu wa mihimili wanateuliwa na M/kt wa chama tawala. Sasa yametimia. Job katoa matamko alioamini yana tija kwa nchi yake, kasulubiwa na washabiki wa chama chake, kagwaya. Yaani, sio wala mashambulizi yaliotoka ofisi ya chama, ni watu wa kawaida tu...wala chama hakikumuita ajitetee popote, kawa mnyooonge, kagwaya. Kaomba msamaha huku akitetemeka kwa unyonge mpaka watu tunatokwa na machozi kwa kumhurumia.
Na yamefumuka mengi, kuhusu chama chake kilivomsaidia kupata uspika/ubunge, kinavomvumilia kwa kuvunja katiba kuhusu wale "Covid 19" ...nk.
Anachosema Spika, kupitia body language, ni kwamba yaliyomtoka kuhusu mikopo, aliropoka tu, hakudhamiria.
Halafu watu wanasifia kuomba radhi kwake kabla hata hajatuhumiwa rasmi na yeyote yule. Wala waliomshambulia hawakuonyesha alipokosea kimantiki, kagwaya. Kiongozi wa Mhimili unamuomba msamaha kiongozi wa mhimili mwingine ili asitimuliwe kazini na kiongozi mwenzake?! Ni Tambo au?!
Halafu wakiambiwa inahitajika katiba mpya, wanaona wanaonewa.