Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

IMG_20220104_000825.jpg
 
Spika amekuwa mnyonge sana lkn ujumbe wke ulifika na kueleweka tunahitaj katiba mpya tumupungizie madaraka rais na kuwa na mihili uhuru bila kuingiliwa hapo tutapata maendeleo ya kweli na utakuwa mwisho ccm
Sasa mlitaka Rais ndiyo awe mnyonge kwa watu wake? Kwa kauli ile angesimamaje kama amiri jeshi mkuu? Acheni hizo, kuomba msamaha kwa watanzania na kiongozi wa nchi ni busara kubwa mno tena hili litamfanya Mh. Rais kuweza kufikiria kama kuna substance katika kauli zile.

Unaweza kuwa na hoja lakini, hoja huwekwa katika context takiwa siyo kudhalilisha na kumwondolea mtu confidence yake na ya watu anaowaongoza. Haifai wala haikiwa ushujaa kukosoana hadharani kama vile mmetalikiana wakati ndoa yenu i hai na mna chumba chenu ambacho mnaweza kumaliza shida na raha zenu pasipo kusumbua public...Tuipende nchi yetu na watu wake
 
Wanasiasa wengi Africa hawawezi kufanya kazi nyingine wakitoka madarakani
 
Ni kati ya fasihi bora kuiona kwenye ulingo wa siasa kwa miaka ya karibuni.
Hii ni namba moja. Ikifuatiwa na ile ya Rutengwe, PhD.
Na kwa bahati mbaya Watanzania wengi hawajui fasihi.
Ngoja tuone upande wa pili wataitikiaje.

Hongera sana kwa Job Yustino Ndugai na kundi lako kwa kuweza kuja na somo bora la fasuhi.
Acha kusifia ujinga Ndungai kama Ndungai, apaswi kuwepo hapo alipo.bunge kalifanya seheme yake ya kupiga pesa, malaya 19 wa kisiasa wanafanya nini bungeni, wanawakilisha chama gani?
 
Leo Spika wa Bunge letu LA JMT Mh Job Ndugai ameongea na vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali ya kibunge na mengineyo.

Moja kubwa lililowagusa wananchi ni kitendo chake cha kumuomba radhi Mh Rais Samia na watanzania wote kwa ujumla kutokana na sintofahamu iliyojitokeza ya kusambaa taarifa mitandaoni za kumkosoa Mh Rais kwa kile alichokiita "Nchi Kuuzwa kwa madeni"

Mm binafsi Nampongeza Mh Spika Ndugai kwa ukomavu wake wa kukiri makosa na kuomba msamaha kwa hilo.

Kuomba msamaha ni jambo dogo sana ila sio wote wanaoweza kufanya hivyo.kuomba msamaha ni kitendo cha kiungwana miongoni mwa waungwana iwe umekosea kweli or hujakosea.

Spika umeonyesha Utanzania wetu ulivyo kwa vitendo.Hongera sana.huu ndio Utanzania tuliorithishwa na wakubwa zetu waliotangulia.

Hapa katikati tulipitia maisha tamaduni na mazoea ya nchi zingine ambazo kimsingi tuliozoea Utanzania wetu tulikuwa tukipata tabu kuenenda na utamaduni Mpya ambao hatukuuzoea.

Watanzania utamaduni wetu ni Kukaa mezani kumaliza tofauti zetu na siku zote anaekubali kushindwa ndie mshindi.kuomba radhi na kukubali kubeba lawama iwe umehusika na kosa unalotuhumiwa nalo or hapana hii ndio sifa ya kiongozi mwenye busara.

Kuna wajinga wengi tu wanakukebehi na kukukejeli kwa kitendo chako cha kuomba radhi,naomba nikutie moyo kwamba tupo sisi ambao tunafikiri nje ya hizo dhihaka na kuona mantiki ya ulichokifanya kwa mustakali mwema wa nchi yetu.

Umeonyesha unazo sifa za kuwa kiongozi mwema,mzuri na unaeweza kubeba mizigo ya watu wengine kwa maslahi mapana ya watu wako.Hongera sana Mh Spika Ndugai.

Miaka ya Nyuma kidogo kwenye miaka ya 1980 Rais mstaafu wa awamu ya Pili Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi,aliwajibika kubeba mzigo wa watu wengine alipokuwa Waziri wa mambo ya ndani kwa kujiuzulu nafasi yake kwa makosa yaliyofanywa na watu wa chini yake.

Inahitaji ukomavu wa hali juu,Uwajibikaji,Busara na hekima kuweza kubeba na kuzikubali "dhambi" hadharani na kuomba msamaha hadharani.kwangu mm hili ni jambo LA kishujaa kwa kiongozi mkubwa kaliba ya Spika wetu.

Huu ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine, kiongozi sio malaika nae ni binadamu kama binadamu wengine hivyo kukosea ni jambo LA kawaida iwe kwa kujua or kutojua.So kitendo cha kuomba msamaha kinaonyesha na kuthibitisha ubinadamu alionao kiongozi.

Nina mengi ya kuzungumzia Ushujaa huu ila naomba niishie hapa, Hongera Mh Spika Ndugai.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Rubbish, akili zako na huyo jamaa zinafanana. Nchi imelemewa na madeni, yani mwaenda kopa mnunue tiles na Mabati ya kijani upuuzi mtupu.
 
Amechanganyikiwa kwani anaona mwisho wake ndio unawadia!!!
hawa wazee wetu ni shida sana,mimi mpaka leo namuheshimu sana yule mzee aliyekuwa msimanizi mkuu wa Hosp ya Dodoma,sijui jina lake,yule alikua anatetea uhalisia bila kumuogopa Boss wake
 
CDF haingilii mambo yao ya siasa aisee hii malumbano huwa hahusiki kabisa anakaaga pembeni kama hawaoni Ila akiona wamezidi yeye hupeleka kikosi ikulu kwamba Sasa naona nchi inawashinda kuendesha wacha niwasaidie.

CDF sio kama unavyomchukulia aisee. Huyo huwa haongei siasa kabisa, muulize Nyerere aliyekumbana na CDF aliyempelekea wajeshi ikulu maana wanadai mishahara yeye alikuwa analeta siasa. Walimnyoosha akamalizana nao fasta kabla hawajalianzisha mtaani.
Tanzania tumekomaa katika governance, otherwise nchi ingeshavurugika hii...Hongereni sana taasisi zetu kwa huu umakini wenu, Mungu aendelee kuwabariki. Naamini kuna sehemu watu saa hizi wamechanganyikiwa zaidi kuhusu nchi yetu
 
Aaaaaaa Ndugai katia aibu ya mwaka. Kalidharirisha bunge na kiti cha u-Spika. Legislature imeufyata kwa Executive 😆😆😆

Naona Ndugai hakumsoma James Montsque aliekuja na dhana ya Seperation of Power and Checks and Balance kati ya; Bunge, Serikali na Mahakama.

Njaa mbaya sana 😆😆😆
Kairudie katiba kwa mara ya pili...Rais ni sehemu ya bunge na ni sehemu ya Judiciary...Kisha ni mkuu wa executives...Hakuna executive yeyote ilishawahi kuwa juu ya Bunge, wala juu ya Judiciary; ila tuna taasisi ya U rais iliyo juu ya zote hizo tatu kwa mujibu wa katiba yetu na ndiyo maana tumeendelea kuwa wamoja, watulivu na hakuna ambaye ameshawahi kuishinda Tanzania...Hakuna template yetu dunia nzima, ndiyo sababu majaribu yote yameshindikana kutuvuruga nchi yetu. Poleni sana wenye uchu wa madaraka na maslahi binafsi...
 
Lakini akina Polepole, Gwajima na Slaa wameonyesha wako ngangali kuliko Spika.

Mkuu wa Mhimili hatakiwi aonyeshe such weakness. Hata kama alikosea angeapologize kiaina siyo direct kihivyo kama mtoto wa shule au raia wa kawaida.
Kiuhalisia wameipunguzia heshima taasisi yake, huu ndiyo ukweli lakini ipi bora, kuupunguzia nchi confidence yake au individuals ambao wameshindwa kuwa wise jinsi ya ku act?

We are growing and learning at same time...Roma haikujengwa kwa siku moja
 
Uoga ni ujinga uliopitiliza na ndio upumbavu wenyewe,but message watanzania wamepata na alichosema ni ukweli na utabaki hivyo deni ndo hilo limefikia hapo hatukujua sasa tumejua hata akiomba radhi but message aliyokusudia imekuwa sent vzr hata waliosema Ndugai aombe radhi wao ndio hawakujielewa kabisa walikuwa wanapoteza muda wao.Siku inakuja MUNGU ataikomboa nchi hii CCM na upumbavu wake imefanya nchi hii inanuka kila aina ya uchafu.
 
Leo Spika wa Bunge letu LA JMT Mh Job Ndugai ameongea na vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali ya kibunge na mengineyo.

Moja kubwa lililowagusa wananchi ni kitendo chake cha kumuomba radhi Mh Rais Samia na watanzania wote kwa ujumla kutokana na sintofahamu iliyojitokeza ya kusambaa taarifa mitandaoni za kumkosoa Mh Rais kwa kile alichokiita "Nchi Kuuzwa kwa madeni"

Mm binafsi Nampongeza Mh Spika Ndugai kwa ukomavu wake wa kukiri makosa na kuomba msamaha kwa hilo.

Kuomba msamaha ni jambo dogo sana ila sio wote wanaoweza kufanya hivyo.kuomba msamaha ni kitendo cha kiungwana miongoni mwa waungwana iwe umekosea kweli or hujakosea.

Spika umeonyesha Utanzania wetu ulivyo kwa vitendo.Hongera sana.huu ndio Utanzania tuliorithishwa na wakubwa zetu waliotangulia.

Hapa katikati tulipitia maisha tamaduni na mazoea ya nchi zingine ambazo kimsingi tuliozoea Utanzania wetu tulikuwa tukipata tabu kuenenda na utamaduni Mpya ambao hatukuuzoea.

Watanzania utamaduni wetu ni Kukaa mezani kumaliza tofauti zetu na siku zote anaekubali kushindwa ndie mshindi.kuomba radhi na kukubali kubeba lawama iwe umehusika na kosa unalotuhumiwa nalo or hapana hii ndio sifa ya kiongozi mwenye busara.

Kuna wajinga wengi tu wanakukebehi na kukukejeli kwa kitendo chako cha kuomba radhi,naomba nikutie moyo kwamba tupo sisi ambao tunafikiri nje ya hizo dhihaka na kuona mantiki ya ulichokifanya kwa mustakali mwema wa nchi yetu.

Umeonyesha unazo sifa za kuwa kiongozi mwema,mzuri na unaeweza kubeba mizigo ya watu wengine kwa maslahi mapana ya watu wako.Hongera sana Mh Spika Ndugai.

Miaka ya Nyuma kidogo kwenye miaka ya 1980 Rais mstaafu wa awamu ya Pili Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi,aliwajibika kubeba mzigo wa watu wengine alipokuwa Waziri wa mambo ya ndani kwa kujiuzulu nafasi yake kwa makosa yaliyofanywa na watu wa chini yake.

Inahitaji ukomavu wa hali juu,Uwajibikaji,Busara na hekima kuweza kubeba na kuzikubali "dhambi" hadharani na kuomba msamaha hadharani.kwangu mm hili ni jambo LA kishujaa kwa kiongozi mkubwa kaliba ya Spika wetu.

Huu ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine, kiongozi sio malaika nae ni binadamu kama binadamu wengine hivyo kukosea ni jambo LA kawaida iwe kwa kujua or kutojua.So kitendo cha kuomba msamaha kinaonyesha na kuthibitisha ubinadamu alionao kiongozi.

Nina mengi ya kuzungumzia Ushujaa huu ila naomba niishie hapa, Hongera Mh Spika Ndugai.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Kwa maana nyingine ameonyesha kuwa Tanzania ni kubwa kuliko individuals, ambaye hatamuelewa hahitaji kuambiwa maana...Bravo Mh. Speaker, umeonyesha maturity ya hali ya juu kuomba msamaha kwa raia wa nchi yako
 
Kama unakamua wananchi kila wakifanya muamala au kununua vocha na kupiga simu sasa mkopo wa nini?

Kama kuna majengo yalikuwa yanajengwa kwa kwa kutumia tozo hizi zinazowakamua wananchi mkopo wa tril 1.3 ulikuwa wa nini?

Japokuwa wananchi wameomba msamaha lakini ujumbe wao umefika murua kabisa.
Mkopo wa trilioni 1.3 ndio umemaliza/unatumalizia changamoto zetu lukuki za kifedha?!!!!

Siempre JMT
 
Kama unakamua wananchi kila wakifanya muamala au kununua vocha na kupiga simu sasa mkopo wa nini?

Kama kuna majengo yalikuwa yanajengwa kwa kwa kutumia tozo hizi zinazowakamua wananchi mkopo wa tril 1.3 ulikuwa wa nini?

Japokuwa wananchi wameomba msamaha lakini ujumbe wao umefika murua kabisa.
Kama huna taarifa sahihi piga kimyaa. Unaonekana Chizi.
 
Kama unakamua wananchi kila wakifanya muamala au kununua vocha na kupiga simu sasa mkopo wa nini?

Kama kuna majengo yalikuwa yanajengwa kwa kwa kutumia tozo hizi zinazowakamua wananchi mkopo wa tril 1.3 ulikuwa wa nini?

Japokuwa wananchi wameomba msamaha lakini ujumbe wao umefika murua kabisa.
TRA wamekusanya trillion 2.51 December pekee, halafu tunakopa trillion 1.3 za kujenga madarasa yenye tiles upunguani hautakaa uishe.
 
Back
Top Bottom