Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Halafu jambo jingine, nitamshangaa sana ndugai asipojiuzulu.......maana si kwa spana zile alizoshushiwa kutoka kule pande za njombe.....
Hawezi kujizulu kwa sasa watampangia muda muafaka.Wakati issue hiyo imesahaulika.
 
Hapo kawafundisha nini wabunge kama spika tu ndio hivyo wabunge wake itakuwa wanasikitisha sana
Lakini akina Polepole, Gwajima na Slaa wameonyesha wako ngangali kuliko Spika.

Mkuu wa Mhimili hatakiwi aonyeshe such weakness. Hata kama alikosea angeapologize kiaina siyo direct kihivyo kama mtoto wa shule au raia wa kawaida.
 
Ujumbe wa Ndugai umefika, sote Kama Watanzania tunalo hitaji la Katiba Bora. Ni aibu kiongozi wa mhimili wa Bunge, kuzodolewa namna Ile na kushawishiwa kuomba msahaha kwa mawazo yake mbadala.
 
Amegongana na mhimili uliojishindilia zaidi, saizi bunge limetolewa fizi kabisa, maana wakati wa hayati liling'olewa meno.......saizi itakuwa praise teams mpaka 2025
 
kuna wasio na jema ambao wao aombe asiombe msamaha ni taarabu tu na kuchamba...hao hata kama ndugu asingefanya chochote wangemshambulia tu....
 
Kama amekosa,ajiuzulu nafasi ya uspika kuonyesha uwajibikaji.
Kama anaamini hajakosa,apige kimya.asubiri wanaomshukia waje apambane.
 
Lakini akina Polepole, Gwajima na Slaa wameonyesha wako ngangali kuliko Spika.

Mkuu wa Mhimili hatakiwi aonyeshe such weakness. Hata kama alikosea angeapologize kiaina siyo direct kihivyo kama mtoto wa shule au raia wa kawaida.
Hao uliowataja hawana privaledge kama za Spika, kama mlikuwa mnadanganyika Ndugai ni mzalendo mlipotea, hapo ni Boss tumbo ndio issue, hayuko tayari kuupoteza uraji wa uspika, kuna pesa ya kufa mtu hapo ofisi ya bunge.
 
MH. NGUGAI AJIUZULU. Baada ya yote haya yaliyo jitokeza baada ya kauli yake atafanyaje kazi na waziri mkuu kwa mfano?
 
Kama siyo Uspika huyu kichaa angekuwa ameshafukiwa kabulini siku nyingi tu.

Hana jeuri hiyo, hata kuropoka kwake ni sababu ya kunyimwa mgao na mama.

Alivyopewa dollar laki moja alikuwa akimsifu mama, leo za Covid hajapewa mgao ndio hasira zake.

Kinachonikera mimi ni Magufuli kutumia pesa za umma kumnunulia mashine ya dayalisis mtu mmoja tena ipo nyumbani kwake, hii ndio siri ya Ndugai kuwa house boy wa Meko.
Kwa hiyo ulitaka nduga afe!!??
acha wivu ww dada
 
Kwa Ndugai kuomba msamaha hadharani kwa matamshi aliyotoa dhidi ya Rais wa JMT, Rais Samia, ni wajibu wa watanzania kumsamehe.
Ndugai ana acute pride, na pride hiyo imetikiswa katika siku hizi mbili tatu.
Pengine alikuwa akijitayarisha kuwaita kwenye kamati yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, lakini kwa muitikio wa hata idara za Chama, Ndugai najua alianza kuona ukubwa unaanza kuota mbawa.

Kwa kuomba msamaha, and eating the humble pie, Ndugai amejishusha na inabidi asamehewe.
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990
View attachment 2067070
Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Huyo hata haeleweki. Ninaona hana tofauti na anaesema kupiga bruce lee kama Van Damme, au wale wanaosema tangu nione sijazaliwa. Fulu kugeuzageuza kauli.
 
Kiongozi wa CCM akiwa nje ya mfumo ni mwepesi kuliko karatasi laini ya chooni.
Rejea Kina Mzee Kinana,Mzee Makamba walivyohenyeshwa na Sukuma Gang,na sasa kina Polepole na Bashiru ni kama watoto yatima.
Ndungai aliliona Hilo akarudi kusujudu mapema asamehewe.Alivyokuwa anatubu ni kama vile alikuwa mbele ya baba paroko!
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990
View attachment 2067070
Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Hili lijamaa ni ng'ombe kweli kweli. Majitu kama hili ndiyo inasababisha wagogo tuendelee kudharauliwa hapa nchini. Bora tu lingekaa kimya kuliko kujidhalilisha kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom