Spika Ndugai ninashauri jaribu kutuliza akili unapotaka jambo liwe

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Na Elius Ndabila

Jana Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai amenukuliwa na vyombo vya habari akisema Serikali iwe makini inapounda timu za kufanya majadiliano ya kimataifa na kupeleka watu makini badala ya wababaishaji.

Mh Ndugai amesistiza kuwa Serikali isiangalie tu kuwa huyu ni Mkurugenzi, RC au Katibu bali iangalie sifa zake alipokuwa shule. Amesema peleka watu waliopata division 1 O level na A level kisha first class degree chuo kikuu hata kama ni vijana wadogo amesisitiza Ndugai. Haijalishi ukurugenzi umeupataje cha msingi ni je una vyeti vinavyoheshimika, amemalizia Spika Ndugai.

Baada ya kusikia nukuu hiyo ya Mh Spika nimejiuliza maswali mengi. Hivi Ndugai hadi leo anaamini division ndiyo inafanya kazi? Hivi Spika anaamini kuwa first class ndiyo inafanya kazi? Maswali yapo mengi ya kumuuliza, lakini ninataka kumweleza Ndugai kazi za dunia ya leo zinataka zaidi juzi, uwezo, uelewa na uzalendo. Kuna watu wana first class lakini uwezo wa ku-argue ni zero kabisa. Kuna watu wana division four lakini wanajua ku-argue kuliko hata hao ambao Ndugai unawataka.

Mh Ndugai anayo mifano mingi ya wazi. Pale Bungeni kuna watu wenye sifa kama anazotaka Ndugai, lakini wana mchango gani? Mimi wakati mwingi ninafurahishwa na Kibajaji, Musukuma, akina Lema ambao shule zao tunazijua kuliko hao ambao leo Ndugai anawataka. Nimthibitishie Ndugai kuna watu wana A, lakini hizo A siyo zao ni za walimu wao au zinatokana na mengi.

Natamani watu wapate nafasi Serikalini si kwa kuangalia vigezo vya Kindugai tu, bali wapimwe zaidi kwa oral presentations. Vyeti vya Tanzania haviaminiki ndiyo maana Mh Rais kwa kipindi chake alikamata watumishi hewa kibao, alikamata waliotengeneza vyeti kibao.

Hivi kama watu walifikia hatua ya kutengeneza vyeti wanaweza kushindwa kujitengenezea A na B? Mh Nugai Bungeni kwake tu ameka na wabunge wengi wenye makalai, lakini hao ndiyo imekuwa msaada kwa Taifa kwa michango yao wanapokuwepo Bungeni. Watu wapimwe kwa credibility na siyo GPA na division.

Ni ushauri wangu kwa Mh Spika kuwa makini sana na kauli zake ambazo zinaweza kugawa watu. Huu ndiyo mtazamo wangu wa watu kupimwa kwa oral interviews na sio kuishia kuangalia vyeti tu. Kuna mtu nilishawahi kusikia kuwa yeye degree na masters alisoma vyote kwa miaka 3 tu.

Pia soma
 
Kwa hili namuunga mkono spika huwezi huwezi peleka watu walio foji vyeti kwenye issue nyeti za kitaifa
Mtu aliyefoji cheti tayari amepoteza uzalendo
 
Spika yuko sahhihi. Pia amefafanua kuwa hao wa Division 1 na First class wawe trained kutusaidia kwenye mambo hayo. Wazo lake ni sawa na tunavyofanya kwa kuwapelekeka watoto wenye ufaulu mkubwa kwenye shule za vipaji. Sasa kwa nini wale wanaofaulu sana vyuo vikuu huwa hatuwachukui na kuwatrain kwenye sehemu nyeti ambazo tunahitaji wataalamu wazuri.

Nchi zote zilizoendelea kama uko smart huwezi kuachwa tu huo mtaani. Watahakikisha unaingiszwa kwnye vitengo maalaumu kama vile Usalama, Foreign Affairs au kwenye special programs za siri jeshini.

Hujawahi kujiuliza ni kwa nini huwezi kuingia kwenye space progam na makarai .... wanaotoaga mifano ya "You don't need a rocket science ....." wana maana yake!!
 
Back
Top Bottom