Spika Ndugai: Nimechaguliwa na watu 400,000 kuwa mbunge kwa miaka 25, mara mbili nimepita bila kupingwa, unaniita ZUZU?

Kupita bila kupingwa ni wizi,ni udhaifu,ni kuchezea akili za watu,huu msamiati umefika mwisho baada ya muasisi wake kufa,2025 hakuna mambo hizo kama ni mwanaume asimame mwenyewe 2025 bila kubebwa kama atapenya.
 
Amechokoza atajuta yete anajiona soeaker bora kuwahi kutokea yaani zuzu wa karne huko komgwa wajitafalari aseee ukute nao vichaa na mazuzu watupu....uĺe ugonjwa umepanda kichwani....sasa
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema anakerwa na tabia ya baadhi ya watu kuwaita wabunge mazuzu na kuwataka wajenge utamaduni wa kuheshimiana.

Amesema yeye amechaguliwa na watu 400,000 kuwa mbunge kwa miaka 25 katika chaguzi mbalimbali na tena mara mbili amepita bila kupingwa.
Ni sifau au aibu kupita bila kupingwa?
 
Hilo Dongo kapigwa Prot Assad

Mwanzo aliwaita Wabunge dhaifu, hivi karibuni alipotakiwa kufanya adjustment ya jina hilo akaiwaita Mazuzu kwa kufanya marekebisho ya sheria kuongeza watu wengine ambao hawatoshtakiwa kwa makosa wayafanyayo wakiwa Madarakani
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema anakerwa na tabia ya baadhi ya watu kuwaita wabunge mazuzu na kuwataka wajenge utamaduni wa kuheshimiana.

Akifungua wiki ya AZAKI jijini Dodoma Jumamosi Oktoba 23, Ndugai amesema, “Sio unaitwa Azaki basi unawasema wenzako maneno unayotaka ya hovyo. Tumewahi kugombana na baadhi ya wazee, mzee unatuita jina sisi hatulipendi…Hivi tumekosea wapi kama unamuita mtu jina la Juma anasema mimi jina hilo silitaki.

“Tatizo lako nini? Unang’anga’ania kuita hilo jina, we ni nani? Haiwezekani kama mwanadamu akikwambia hiki sina raha nacho kiache na wewe hukiachi, kama kweli wewe ni muungwana mtu wa Mungu utakiacha.”

Amesema matokeo ya kutoheshimiana ni wazee (ambao hakuwataja) wanawasema wabunge ni mazuzu wakati wana akili.

Amesema wao hawana muda wa kubishana bishana na watu wana namna hiyo.

Amesema yeye amechaguliwa na watu 400,000 kuwa mbunge kwa miaka 25 katika chaguzi mbalimbali na tena mara mbili amepita bila kupingwa.

“Hata kesho nikienda kusimama (kugombea) tafuta wa kusimama na mimi hutampata. Akisimama ni mpambe wa kusindikiza. Halafu wewe unaniita zuzu yaani wale watu una maanisha ni mazuzu wamechagua zuzu mwenzao?”amehoji.

Ndugai alipongeza Azaki kwa kazi nzuri wanazofanya lakini akasema wachache wao wamekuwa wakitumika na wana ajenda zisizokuwa za kwao na kwamba Azaki chache zimekuwa na ajenda za kupata fedha kutoka mahali fulani (hakukutaja).

“Sasa kama we njaa yako ni hela ndio maana lazima zitungwe sheria sasa zinazokufuata kwenye hela. Eeeeh utatuambia nani amekupa, kiasi gani, ziko wapi, utazitumiaje na utaleta taarifa kwa kila shilingi zamani haikuwa hivyo tuliaminiana lakini baada ya kuona mwenendo usio ridhisha ndio tukatunga sheria,”amesema.

Ndugai amesema kama wasipoweka sera ya kuambiana na kurekebishana (wao kwa wao mashirika) basi hata sheria zitakazotungwa siku za usoni zitakuwa kali zaidi.
Mtu unajisikia kuchaguliwa na wajinga laki nne
 
Kweli kila zama na kitabu chake. Leo hii Ndugai anapiga yowe bila kuchukua hatua zidi ya Assad,ingekuwa kipindi cha Kayafa sasa hivi Assad angekuwa mikononi mwa Polisi kwa amri ya Ndugai. Haya ni maneno ya Ndugai.

"Kuna Mzee anatukosea sana Wabunge,anatuita mazuzu,nina miaka 25 pale Kongwa na vipindi viwili nimepita bila kupingwa,na hata kesho nikienda nitapita bila kupingwa,kwanini uniite zuzu? Wananchi wa Kongwa ni mazuzu wamechagua zuzu mwenzao?"

Credit: Dar Mpya.
 
Leo imenicjekesha Sana Bwashehe!!
Lakini amesema amechaguliwa na mazuzu 400000 Kwa miaka 25 tena mara 2 Hakuna zuzu aliyejitokeza kupambana naye. Wilaya ya mazuzu.
Hahahaaaa... Zamani ukiona mbunge anapita bila kupingwa ujue ni Mchawi!
 
Back
Top Bottom