Spika Ndugai: Nassari miezi tisa hajafika bungeni, wala hatuna barua yake hata barua aliionesha haina sahihi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
Habari wakuu,

Spika anasema Nassari hana sifa ya kuendelea kuwa Mbunge, Hajahudhuria mikutano waka kikao chochote kwa miezi tisa mfululizo.

Spika anasema "Labda nifafanue kwa Watanzania, kuna neno Kikao na neno mkutano. Mkutano ni ule mmoja ambao unakuwa na urefu wake mzima. Kama huu ambao tunauanza na tumeshaanza kamati zake, huu ni mkutano wa 15. Yaani kwa Mwaka mmoja tuna mikutano minne. Kila mkutano mmoja katika hiyo minne ukifanyika kwa siku 10 basi kuna Vikao 10, ukifanyika kwa siku 40 basi huo mkutano utakuwa na vikao 40. Ndo tofauti ya Mkutano na Vikao.

Kwahiyo yeye Mheshimiwa Nassari hakuhudhuria Mikutano Mitatu. Kwa Mwaka tuna Mikutano minne, kwahiyo ndo kusema kwamba Nassari hajahudhuria Kamati au Bunge lenyewe kwa miezi tisa mfululizo. Kwakweli katika Maisha ya kawaida, mtu uliyepewa jukumu la kufanya tena umepewa na wananchi, umeaminiwa na wananchi halafu wewe kwa miezi 9 mfululizo huhudhurii kikao chochote cha kamati wala cha bunge lenyewe, Halafu ukiulizwa unasema ulikuwa unauguliwa, kwakweli kidogo sidharau kuuguliwa. Taratibu zinasema kama una jambo la dharura toa taarifa kwa Spika, Sikuwa na taarifa yoyote inayohusu zuio la yeye kutokuhudhuria bunge kwa miezi tisa, ni muda mrefu sana hata kama kuna tatizo bunge lingejua'" Amesema Spika Ndugai.


Spika akaendelea kusema, "Nimeona barua ambayo hata haijasainiwa, na hata kwenye mafaili yetu barua hiyo haipo na huo sio utaratibu. Hakikisha Spika anapata taarifa, maana yake mpe barua kwa dispatch Spika mwenyewe, wao wapo kwenye chama cha siasa na chama chake ni chadema, na wana kiongozi, kiongozi wake angenipa taarifa ya mwenyewe, naibu kiongozi angenipa. Hakuna aliyenipa taarifa yoyote kwa miezi tisa. Kwahiyo hajaonewa na mtu yoyote hayo ni maneno ya Mkosaji.

Ni kweli wakati nampa hizi taarifa alikuwa kwenye kamati ya bunge anafanya kazi kule Moshi. "Hiyo ni kweli. lakini hiyo haihesabiki katika vile vikao vyangu ambavyo kikatiba vinamtaka. Hiki ndio kikao cha nne cha Mwaka. Katiba inasema ukikosa mikutano Mitatu, yeye alishakosa mitatu, hata kama huu ningemruhusu ahudhurie mpaka mwisho, bado angekuwa hana sifa kwa vile mikutano mitatu kwa miezi tisa hajahudhuria bunge wala kamati yake wala kureport chochote kwa Spika, wala hana barua ya Spika ya kukiri kupokea barua au chochote kutoka kwake. Wala hana barua ya Spika ya ruhusa ya hilo jambo alokuwa akiliombea." Kafafanua Spika Ndugai.

Habari zaidi, soma=>Joshua Nassari avuliwa Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa “Utoro” Bungeni - JamiiForums

Mbunge Joshua Nassari amehitimu masomo yake Shahada ya uzamili, MA International Relations & Democratic Politics. - JamiiForums

Joshua Nassari: Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti - Maisha yangu yapo HATARINI Watesi wetu wananitafuta - JamiiForums
Mbunge Viti Maalum CCM, Amina Mollel adai Mbunge Joshua Nassari hajui shida za waliomchagua - JamiiForums
 
At least to its minimum angefuata procedure za kumsikiliza na kumjulisha hiyo nia yake ya kumvua ubunge. ......bas hata barua angepewa yeye kwanza. ...
Mr speaker. .... vipi angekuwa wa chama chako, Ungefuata utaratibu huo?

Anyways... bado namuona Nassari anayo shida ya msingi kabisa. ..
9 month bila kwenda kazin. ....dah.....
 
Nassari inabidi arudishe Mishahara ya Miezi tisa aliyokula bila ya kufanya kazi

Alikuwa Mbunge Hewa
Je wajua waziri wa sasa wa katiba na sheria ndiye anayeongoza kwa utoro bungeni kuliko mbunge yeyote???
Hili hata spika alilisema,je,kuna hatua zozote zilizochukuliwa?
 
Hata awe Na Kiinua Kiuno Haina Shida cha msingi aoneshe uadilifu kwa kurudisha pesa aliyokula bila ya kufanyia Kazi
ndio mnanyoosha etieee
IMG-20190313-WA0058.jpg
Screenshot_2019-03-13_184217.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
naombea upate mimba ijayo utoe huyu anefanana na yuleeeView attachment 1046682

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimeshatilisha Mimba kwa zaid ya Miaka 40 na sasa nakula Penshen

Mimba ya Mwisho nimetilisha wakati huo Rais wa Marekan Ni Bill Clinton Na Rais wa Kenya Ni Daniel Arap Moi, Burundi Ntaryamira, Rwanda Habyarimana, Zaire Mobutu Seseseko, Zambia Chiluba, Malawi Dkt Kamuzu Banda, Msumbiji Chissano!

Dua yako ime expire tayari kabla hujamaliza kuomba
 
Back
Top Bottom