Spika Ndugai na wabunge Wanawake (Viti Maalum)

Kwa miaka kadhaa, kumekuwa na minong´ono kuhusu mahusiano ya Mbowe na wanawake wanaotaka kuchaguliwa kwenye nafasi za viti maalum bungeni kwa tiketi ya chama cha Mbowe. Wapo wanaosemekana hata kumzawadia watoto.
Ila siku zote mamlaka za nchi hazijawahi kulitolea neno. Wakati wa ile kampeni iliyoanika matatizo ya ngono lazimishi wanawake wanazokutana nzao makazini na mashuleni/vyuoni, cha ajabu wanasiasa walikuwa kimya.

Lakini leo kwa mara ya kwanza nimemsikia Spika akiongea kuwa humo mjengoni hakuna siyejua shida wanazopitia wabunge wa viti maalum wa Chadema.

Imekuwa siri ya wazi na iliyokubalika kwa jamii kuwa ukitaka viti maalum Chadema, lazima Mwenyekiti na kambi yake waridhishwe na wewe.

Ila leo ndo mara ya kwanza kumsikia mkuu wa mhimili husika, kuashiria kujua hivyo viti maalum vinagawiwa kwa vigezo gani, ambavyo ni kinyume na katiba.

Swali langu kwa Spika;
Je, anaona ni sahihi kwa kiti chake kufumbia macho hilo swala?

Kama mzazi mwenye watoto wa kike na kiongozi mkuu wa huo mhimili, amechukuwa hatua gani kuwalinda hao akina dada na wadada wajao dhidi ya ukatili huo?

Mbowe je, uchaguzi huu wa 2020 atabadili vigezo au wembe ni ule ule?
Bila shaka watajitokeza watakao thibitisha maneno ya Spika.

Amandla...
 
Zamu hii kaingia kwenye 18 za Job!

Chadema itabaki na Mbowe, Mdee na Heche tu!

..wamuwekee mtego kama wa Dr.Slaa.

..au wamdukue kama walivyomfanyia Mzee Makamba.

..ila wakati mwingine ukimuandama sana mtu unaweza kusababisha jamii ikaanza kumuonea huruma.
 
Back
Top Bottom