Spika Ndugai na Mwambe wapewa wito wa Mahakama, kesi kuanza Juni 3

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Kesi namba 12/2020 inayomkabili Spika wa Bunge, Job Ndugai imepangwa kuanza kusikilizwa Katika Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es salaam mnamo Juni 3 mwaka huu kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa Saba.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa na Taasisi ya Haki za Kiraia na msaada wa Kisheria(CILAO) inaiomba Mahakama kutoa tafsiri kuhusu kitendo Cha Spika huyo kumruhusu Mbunge wa Ndanda, Mwambe kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge ilhali alishatangaza kuhama Chama chake na kuhamia CCM.

Zaidi, soma: Kesi dhidi ya Spika Job Ndugai na Cecil Mwambe kutajwa kesho. Ni ile ya kuomba tafsiri ya Mahakama baada ya Mwambe kurudishwa Bungeni
 
Mwambe anawatesa sana ufipa! Kichwa cha nyoka hakibebi mzigo, by Mustafa Muro.. DJ ana akili ndg
 
Mwambe anawatesa sana ufipa! Kichwa cha nyoka hakibebi mzigo, by Mustafa Muro.. DJ ana akili ndg
Mwembe sio tishio, CDM na Mbowe wapo salama na wasafi, wangekuwa na kasoro ama madudu Makatibu wabuu wakuu Slaa na Mashinji wangetumika ipasavyo.
 
Huwezi kuamini kitendo cha wale wananchi kusema vile mbele ya Rais, akirudi kongwa wakati wa kampeni anaweza kumponda Ndugai hapo hapo
Mwisho wa Ndugai ni aibu kubwa. Kitendo cha wakazi wa Kongwa kumkataa mbele ya Rais ndio mwanzo wa mwisho mbaya
 
No one should be condemned unheard... hata kama kavunja Sheria wazi wazi.

Good move! That's the right path... rather than condemning one through vijiwe vya kahawa.

Principle of natural justice observed.

Will the justice be dispensed? Hili ni suala jingine ambalo might draw both 'Yes or No'. However, kibongo bongo, penye YES panaweza wekwa NO.

-Kaveli-
 
Na yeye kaanza kuangaika na kwenda mahakamani ndio malipo ya kumtumikia shetani. Anakutumia then anakubwaga. na bado tutaona mengi hata usipika haupo atafute kazi ya kufanya 2020~2025.

Mkuu kwani Ndugai yeye ataenda mahakamani au ni wanasheria wa bunge? Halafu viongozi wa kiafrika huwa hawaogopi mahakama, bali huogopa nguvu ya umma tu.
 
Huyo Ndugaye naona sasa anatafuta kwa nguvu kumuachia joho Betina

Back
Top Bottom