Spika Ndugai na Katibu wa Bunge wapelekwe Mahakamani kwa kutoiheshimu Katiba waliyoapa kuitetea

Kutoheshimu katiba ya nchi unayo apa kuifuata na kuilinda ni kosa kubwa la pili baada ya uhaini na mauaji.

Spika wa Bunge Job Ndugai na Katibu wa Bunge wanapaswa kupelekwa mahakamani kama sio leo basi baada ya utawala huu unaowalinda kuondoka madarakani.

Sakata la Wanachama wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama na kuendelea kuwa wabunge kinyume na maelekezo ya katiba ni kuidharau hiyo katiba na kwa maana hiyo ni kosa kubwa la jinai linalofanywa kwa makusudi.

Kama Spika wa Bunge hawezi kuheshimu katiba kuna sababu gani raia wengine kuiheshimu?
Wapeleke wewe nani awapeleke sasa?
 
Back
Top Bottom