Spika Ndugai na Katibu wa Bunge wapelekwe Mahakamani kwa kutoiheshimu Katiba waliyoapa kuitetea

MtuHabari

Senior Member
Oct 16, 2020
158
500
Kutoheshimu katiba ya nchi unayo apa kuifuata na kuilinda ni kosa kubwa la pili baada ya uhaini na mauaji.

Spika wa Bunge Job Ndugai na Katibu wa Bunge wanapaswa kupelekwa mahakamani kama sio leo basi baada ya utawala huu unaowalinda kuondoka madarakani.

Sakata la Wanachama wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama na kuendelea kuwa wabunge kinyume na maelekezo ya katiba ni kuidharau hiyo katiba na kwa maana hiyo ni kosa kubwa la jinai linalofanywa kwa makusudi.

Kama Spika wa Bunge hawezi kuheshimu katiba kuna sababu gani raia wengine kuiheshimu?
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,157
2,000
190876.jpg
 
std7

JF-Expert Member
May 6, 2011
633
1,000
Spika ana kinga ya kutokuishitakiwa, na hiyo kinga walijiwekea na wabunge wa ccm kuipitisha, ili spika aikanyage katiba vizuri.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
26,754
2,000
Spika ana kinga ya kutokuishitakiwa, na hiyo kinga walijiwekea na wabunge wa ccm kuipitisha, ili spika aikanyage katiba vizuri.
Akiingia Lisu, say, watafungwa maana hatuwezi kukubali sheria ya kishenzi ya kulinda maovu. Tutaunda mahakama maalum nje ya mahakama hizi za sasa kushughulika na waasi hawa waliojiwekea sheria ya kujilinda ili wafanye maafa
 
MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,606
2,000
Kutoheshimu katiba ya nchi unayo APA kuifuata na kuilinda ni kosa kubwa LA pili baada ya uhaini na mauaji....
Chadema ilitoa fursa ya waliofukuzwa kukata rufaa na kwa mantiki hiyo hukumu ya kamati kuu haikupelekwa kwa spika mpaka Baraza kuu litakapokaa na kuisikiliza rufaa ya wanachama 19.

Mpaka hapo mpira uko miguuni mwa Chadema,Baraza kuu litabariki maamuzi ya kamati kuu na kumuandikia spika au baraza kuu litawasamehe na kuwarudishia uanachama wao,NI suala la muda.

Mpaka sasa Ndugai yupo huru kufanya lolote na hao wabunge 19!

Ni kwa uelewa wangu!!
 
Duniahadaa

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
317
1,000
Chadema ilitoa fursa ya waliofukuzwa kukata rufaa na kwa mantiki hiyo hukumu ya kamati kuu haikupelekwa kwa spika mpaka Baraza kuu litakapokaa na kuisikiliza rufaa ya wanachama 19..
HUKUMU HAIKUPELEKWA! NANI MKWELI KATI YAKO NA NDUGAI ALIYESEMA ALIIPATA ILA AKAAHIDI KUWALINDA?
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,345
2,000
Nawaonea huruma sana wazee wajinga hawa! Hivi hawajihurumii wao na familia zao? Wanajua uchungu watakao pata watoto wao wakiona wazee wao wako jela kwa makosa ya kujitakia yasiyo na faida?
Mkuu una angalizo zuri, ila matamanio yako sio rahisi kufikiwa kwani ukija utawala mwingine watasema hawafukui makaburi.
 
MAGALEMWA

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
6,238
2,000
Chadema ilitoa fursa ya waliofukuzwa kukata rufaa na kwa mantiki hiyo hukumu ya kamati kuu haikupelekwa kwa spika mpaka Baraza kuu litakapokaa na kuisikiliza rufaa ya wanachama 19....
Uko sawa, ila niambie hata mishipa ya fahamu hawana kuwa katiba inavunjwa?
 
Ndamwe

Senior Member
Jun 11, 2008
158
225
Kutoheshimu katiba ya nchi unayo apa kuifuata na kuilinda ni kosa kubwa la pili baada ya uhaini na mauaji.

Spika wa Bunge Job Ndugai na Katibu wa Bunge wanapaswa kupelekwa mahakamani kama sio leo basi baada ya utawala huu unaowalinda kuondoka madarakani.

Sakata la Wanachama wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama na kuendelea kuwa wabunge kinyume na maelekezo ya katiba ni kuidharau hiyo katiba na kwa maana hiyo ni kosa kubwa la jinai linalofanywa kwa makusudi.

Kama Spika wa Bunge hawezi kuheshimu katiba kuna sababu gani raia wengine kuiheshimu?
Walishajiwekea kinga
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom