Spika Ndugai Msaidie Rais Magufuli kwa kuzuia walevi wasiingie Bungeni

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Kwanza kabisa napenda kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua dhidi ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya Bwana Kitwanga kwa kwa kosa la ulevi wakati wa kazi, hii imeonyesha dhahiri kuwa Rais Magufuli ni Rais wa anatembea na maneno yake ya kuwa anataka kazi tu na wala si masihala na hana simile na yeyote yule anayeleta mzaha katika kazi bila ya kujali nafasi yake ya kisiasa au ya kijamii

Ni Rais asiyetaka mchezo mchezo katika mambo yanayohusu maslahi ya taifa, Magufuli ameonyesha anaweza kufanya zaidi ya watangulizi wake katika kusimamia nidhamu na maadili serikali, ameonyesha asiyetaka uswahiba katika mambo ya uongozi wa nchi.

Watanzania kwa ujumla wetu tumsaidie Rais katika kuwatumbua walevi wengine katika maeneo yetu ya kazi pamoja na sehemu zenye huduma za kijamii kama ukienda ofisi unampokuta mlevi haraka sana yafaa kuripoti ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.

Waheshimiwa kama kitwangwa wapo wengi sehemu za kazi, na hata bungeni tuwatumbue tu bila ya kuwaonea haya kama alivyofanya Rais Magufuli ili kuwatoa wazembe na wasiowajibika ili nchi yetu isonge mbele.

Natoa rai kwa ofisi ya bunge kuweka vitaa vya utambuzi kwa wanaokunywa pombe na kuingia ndani ya bunge, bunge linapaswa kuhakikisha mheshimiwa yeyote alikunywa pombe asiingie ndani ya bunge na hapo ndipo tutakaa sawa na kudhibiti walevi maeneo ya kazi.

Haiwezikani na si halali hata kidogo waheshimiwa wetu kutufanyia dhihaka ya ulevi ndani ya bunge letu kwa kuingia wakiwa tirarila nia aibu kwa taifa,

Pia nanyi waheshimiwa hebu jiheshimuni na mjipime kwa matendo yenu, haiwezekani tunawalipe, mamilion kwa kodi zetu na magari ya bei mbaya halafu mnatufanyia uhuni haiwekani hata kidogo.

Namuomba Spika Ndugai alisimamie hili la kuhakikisha walevi hawaingii bungeni kwa kufunga vifaa vya utambuzi kwa walevi
 
Unachojaribu kukifanya ni kama kosa tulilowahi kufanya kwny harusi moja tulipomteua Kitwanga mmoja wapo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Vinywaji. kabla hata harusi haijaanza tayari yeye yupo Mbende mbende hajielewi kabisa.

Kumshauri Job kuzuia Wabunge walevi kuingia Bungeni ni sawa na kusababisha akidi kutokutimia ikiwa ni pamoja na kumzui Spika Mwenyewe kuingia Bungeni!! mpaka Bhangi wanakula kwa mujibu wa Mbunge wa Geita Mh. Msukuma!
 
Nadhani tatizo la ulevi wa bangi kwa wabunge wakiwa katika kazi zao za kibunge ni kubwa kuliko ulevi wa pombe.
 
Nimeona video ya kitwanga - kweli inaonesha hakuwa sawa - lakini kabla ya utumbuzi nani kahakikisha kuwa alikuwa kauchapa ? au ni matatizo ya kiafya kama matumizi ya dawa nk
 
ni sawa. kosha la ulevi kazini ni kosa la kisheria na kinidhamu.
tusimsubiri rais kwa kila jambo
 
Bunge linaendeshwa kwa kanuni ndugu na sina hakika kama kanuni ya ulevi wanayo.
 
Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema ameshauri vifaa vya kupima ulevi kama vile wanavyopima navyo madereva viwekwe katika mlango wa kuingia bungeni ili kila waziri na mbunge apimwe kabla ya kuingia bungeni. Ameyasema hayo alipokuwa anaongea na ITV.

Nini maoni yako?
 
CcM walikuwa wakisema kuwa CDM ni wanywa viroba ona sasa kumbe tuna mawazir wanywagongo.
Yule kwa hali aliyokuwa nayo nisingeshangaa kama "angechomoa" na kupunguza mzigo pale pale live. Cheza na kilevi wewe.
 
Wazo zuri ila alikuwa wapi mda wote asitowe hayo mawazo siku zote alizo kuwa bungeni.
 
Anafaham yeye ni mlevi ndio maana amesema kifaa kiwekwe kwa mawaziri tu na sio wabunge...
 
Back
Top Bottom