Spika Ndugai: Mnaogopa nini kuleta viambatanishi ili tuwavue Ubunge kwa Haki?

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,149
12,818
Spika Job Ndugai ameendelea kutoa ufafanuzi juu ya utaratibu wa kuwavua ubunge wabunge 19 wa viti maalumu wa CHADEMA, Mh Spika ameendelea kusisitiza kuwa anaongoza Bunge kwa Katiba, Sharia, Kanuni, Hekima na Utamaduni ili kutenda haki.

Mhe. Spika amevitaka vyama vya siasa pale wanapotaka kuwavua uanachama wabunge yawapasa kuambatanisha Katiba ya chama chao pamoja na Muhtasari wa Kamati Tendaji ya chama iliyofanya maamuzi ya kuwavua uanachama wabunge wanaopaswa kuwafukuza ili naye apate kujilidhisha kama utaratibu ulifuatwa na atende haki pasi kumuonea mtu yeyote.

Mhe. Spika ameongeza kuwa kwa mujibu uo atafanyakazi pia na msajiri wa vyama vya siasa maana yeye ndo ana Katiba za chama na kila wanapofanya mabadiliko ya Katiba kwenye vyama ua anapelekewa nakara za katiba ambazo ni latest.

Mhe. Spika amemalizia kwa kuhoji kwanini Chadema hawapeleki hizo nakala? Wanaogopa nini?

Mpaka hapo inaonesha wazi spika anajua chadema walikosea wapi kisheria ndio maana kila siku anawataka wapeleke.

Maybe kwenye hiko kikao akidi ilikuwa haijatimia au kuna mapungufu kutokana na Katiba yao.
 
Huyo ni Ndugai.. Ati spika wa bunge linalo tunga sheria.

Halafu yeye hajui sheria.

Kama ameleta kanuni zinaanza leo na siyo nyuma

Hivi alishindwa nini kuwa pigia Chadema simu alipo pata barua yao miezi mitano iliyo pita? Ati leo ndio ana simama na kutoa

Maelekezo ya kipuuzi?

Screenshot_20210507-125826.jpg
 
Me nafikir ifikie wakat mambo ya kiofisi yapelekwe kwa taratibu za kiofisi, na hyo ndio professionalism.

Hivi spika aliwajibu CHADEMA ya kuwa barua waliyoiandika haikua barua ila kimemo?

Hivi taratibu alizozizungumzia na anazoendelea kuzizungumzia ya kwamba CHADEMA imewapasa kuzifuata anawaelekeza anapokua katika kiti chake Bungeni au amewaandikia official letter ili kuwajuza viongozi husika?

Bwana Job Ndugai, Bungeni sio sehemu ya kufanyia taarabu na propaganda. Waeleze hayo yote kupitia official letter na sio Bungeni!
 
Huyo ni Ndugai.. Ati spika wa bunge linalo tunga sheria.

Halafu yeye hajui sheria.

Kama ameleta kanuni zinaanza leo na siyo nyuma

Hivi alishindwa nini kuwa pigia Chadema simu alipo pata barua yao miezi mitano iliyo pita? Ati leo ndio ana simama na kutoa

Maelekezo ya kipuuzi?
View attachment 1776270
Huyu naye kaanza kuharisha humu jukwaani anashindwa kuchunga kondoo anakuja kwenye siasa
 
Kwani ni nani aliwateua kuwa wabunge?
Mkuu umeuliza awali zuri sana na wengi wanalikwepa. Je uteuzi wa wabunge ukifanywa na mamlaka sahihi?? Kwa sababu Ndugai anajifanya hajui walifukuzwa kwa sababu gani. John Mnyika anadai vikao husika havikuwateua hawa kuwa wabunge - anadai waligushi!! Na kufukuzwa kwao ni kwa sababu wabunge hawa walipoka mamlaka na kujiteua.

Ni vema kujua kama waliteuliwa au walijiteua!
 
Kwa kuwa kila upande umeshupaza shingo na kuendelea kujihesabia haki, hili saga linaweza kwenda mpaka Oct 2025.
 
safi sana spika kama wanashindwa basi hawana nia ya kuwavua uanachama na kama hawaleti vielelezo basi kuna sehemu wamebugi sana wanaona wakileta tu kimewanukia siyo myika kwa kuwa aliambiwa na mdee kuwa alikuja na ndala chadema basi ndiyo anataka kumrudishia kwa hapo amenoa walete viambata
 
John Mnyika anadai vikao husika havikuwateua hawa kuwa wabunge - anadai waligushi!! Na kufukuzwa kwao ni kwa sababu wabunge hawa walipoka mamlaka na kujiteua.
Ndugai kajificha chini ya kivuli cha NEC maana majina ya Wabunge yanatoka NEC. Hili swali hata Ndugai mwenyewe atalirefer kwa NEC

Kwenye hayo madai ya forgery nadhani hata NEC wanaweza kujitoa ufahamu na kuitaka CHADEMA ikaithibitishe hiyo forgery kortini
 
Mkuu umeuliza awali zuri sana na wengi wanalikwepa. Je uteuzi wa wabunge ukifanywa na mamlaka sahihi?? Kwa sababu Ndugai anajifanya hajui walifukuzwa kwa sababu gani. John Mnyika anadai vikao husika havikuwateua hawa kuwa wabunge - anadai waligushi!! Na kufukuzwa kwao ni kwa sababu wabunge hawa walipoka mamlaka na kujiteua.

Ni vema kujua kama waliteuliwa au walijiteua!
hapo ndiyo kwenye shida kuu kwanini mbowe yuko kimya sikuhizi anajuwa nani alipeleka majina sasa hawa wakienda kwenye rufaa tu kimenuka ndiyo maana hata rufaa hawataki utashtukia imefika 2025
 
Ndugai kajificha chini ya kivuli cha NEC maana majina ya Wabunge yanatoka NEC. Hili swali hata Ndugai mwenyeww atalirefer kwa NEC

Kwenye hayo madai ya forgery nadhani hata NEC wanaweza kujitoa ufahamu na kuitaka CHADEMA ikaithibitishe hiyo forgery kortini
yes wamepeleka majina wenyewe halafu wanayakana waende mahakamani wakaseme wamefogiwa
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom