Spika Ndugai: Mkiniona naharibu alaumiwe Makinda

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Kauli hiyo ameitoa Bungeni Dodoma, jana jioni Juni 10, 2021, wakati akimkaribisha Bungeni, na kuongeza kuwa Mama Makinda, amekuwa ni mwalimu wake kwa kipindi kirefu tangu alipoingia Bungeni kwa mara ya kwanza.

"Mama Makinda amekaa humu Bungeni takribani miaka 40 hii rekodi siyo rahisi na yeye alikuja kama mbunge kijana, nilipoingia hapa Bungeni nilipangwa kwenye Kamati ya Ardhi Maliasili na Mazingira na yeye akawa ni Mwenyekiti wangu, miaka mitano iliyofuata yeye akawa Mwenyekiti wa Bunge mimi akaniachia kijiti kwenye kamati,"amesema Spika Ndugai.

"Baadaye akawa Naibu Spika mimi nikawa Mwenyekiti wa Bunge yeye akawa Spika wa Bunge mimi nikawa Naibu Spika, ameenda kustaafu nimekuwa Spika kwa hiyo mimi huwa nafuata mguu wake anapotoa mimi naweka sasa kwa vile alishastaafu na mimi nafuatia nitakuja kuwaambia huko mbele, namshukuru sana Mama kwa malezi mkiniona naharibu alaumiwe yeye maana yeye ndiyo mwalimu wangu kila hatua," ameongeza Spika Ndugai.
 
2797542_IMG-20210604-WA0005.jpg
 
Hapo mmechemsha hajavunja katiba nyie ndiyo mnafanya uhuni mtawafukuzaje watu kihuni namna hiyo? Mbowe mtambo kweli
Mkuu unaongea ukiwa unajua katiba inasemaje kuhusu wabunge wa viti maalum ?watu wengine ubongo unakuwa kichwani ila wewe ubongo wako upo makalioni
 
Back
Top Bottom