Spika Ndugai: Mbunge yoyote anayejihisi ana dalili za Corona ajifanyie Self Isolation na kuripoti hospitali haraka sana!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,852
141,786
Spika wa bunge mh Ndugai amesema endapo mbunge yoyote anajihisi au atajihisi ana dalili za maambukizi ya Covid 19 kama zilivyoainishwa na wataalamu wa afya basi ajifanyie self isolation na kuripoti hospitali haraka sana.

Spika Ndugai ametoa mwongozo na tahadhari hiyo Bungeni leo hii na amesisitiza sana na kurudia rudia kwamba wabunge wenye dalili za maambukizi ya Covid 19 " WASISITE" kujiweka katika Karantini.

Source Clouds tv!
 
Kuna mtu kakinukisha bungeni
Mbowe, mbunge wa kinondoni, Rwakatale mh nawaza tu
 
Kwanini wasiwapime wote? Kusubiri mpaka mbunge aonyeshe dalili si atakua kambukiza wengi

Kwanin serikali ya awamu ya tano hainunui magari ya vipimo mengi iwezekanavyo kama south afrika ili watupime kwa wengi iwezekanavyo mtaani?

Rais wetu wa wanyonge yupo wapi? Yeye ndio mfariji wa taifa, tunaitaji kusikia sauti yake ya faraja ikiwezekana kila siku itwapo leo
 
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwapima wabunge wote ni njia nzuri ya kujua ukubwa wa tatizo nchini na wale positive watakaa umwali kupunguza ukubwa wa tatizo
 
Hawa watawala ni MBUMBUMBU kwelikweli. Hivi Nchi hii ina sheria na taratibu mbili tofauti: kwa wabunge tu na kwa raia wanyonge?

Baada ya naibu speaker kuconfirm kwamba kuna mbunge mmoja ametest COVID19 positive, wabunge wote wanaohudhuria bunge walipaswa kuwa isolated/kuwekwa quarantine ya lazima kwa siku 14 na woooote wapimwe angalau mara mbili within those 14 days. Hii ya kuishi kwa mazoea tu huku "tukiomba na kusali" baa lipite pembeni ni dalili za ujima hizi.
 
Wengine hawana dalili ila wanaambukiza tu. Hapo ndo kwenye Puzzle yenyewe. Cha muhimu wapimwe tu kwanza.
Hata kupimwa hakusaidii. Tena kunaleta confidence mbaya na ya hatari ambayo inaweza kusababisha maambukizi zaidi. Imagine mtu akipima leo akikutwa hana kumbe wale virus aliambukizwa siku moja au mbili zilizopita? Nikupe mfano mmoja. Ndege ya mwisho ya Kenya Airways kutoka USA kabla hawajasitisha safari za USA ilirushwa na rubani mmoja anaitwa Daudi Kibati.

Ilipofika Nairobi siku ya safari ya mwisho, ilibidi akae karantini kwa sababu alikuwa ametoak USA iliyokuwa na maambukizi mengi. Baada ya siku tatu wakam-test virus akawa hana lakini ikabidi akae karantini mpaka siku 14 ziishe. Siku ya tano wakam-test ikawa negative tena.

Kufika siku ya tisa akaanza kuumwa na alipofanyiwa test ikawa positive na kufariki siku tatu baadae. Njia nzuri ya Bunge kufanya ni kukatiza vikao mara moja mpaka hali itakapokuwa nzuri.
 
Wengine hawana dalili ila wanaambukiza tu. Hapo ndo kwenye Puzzle yenyewe. Cha muhimu wapimwe tu kwanza.
hao besti wanaitwa 'superspreader' kuna waliotoka nayo swiss alps January wakarudi Norway wameambukiza balaa. Wahanga wanadai wanafeel vitu kama vipande vya chupa vinasimikwa na kuchomekwa kooni na mapafuni.
 
Hao ndo wakuogopa zaidi. Ndo umuhimu wa security distance unakuja. Kukaa mbali na binadamu mwenzako.
 
Viongozi wetu Tanzania wamepigwa upofu...wanafanya Mambo kinyume...Kuna sababu kiroho naamini hivyo.
 
Back
Top Bottom