Spika Ndugai: Mbunge wa Kigoma Mjini,Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) anawadanganya wananchi kuhusu ripoti ya CAG

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890

Spika wa Bunge Job Ndugai,amesema Mbunge wa Kigoma Mjini,Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) anawadanganya wananchi.

Ndugai alisema uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), unaofanywa na Zitto unalenga
kuwaaminisha wananchi kwamba kila kilichomo kwenye ripoti hiyo ni cha kweli.

Alisema kwa upande wake humuungi mkono kwa kuwa ukweli wa ripoti hiyo hudhihirishwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni kamati ya PAC na LAAC.

Spika Ndugai aliyasema hayo bungeni leo mchana muda mfupi kabla hajaahirisha Bunge hadi jioni.

Pamoja na hayo Spika alisema Zitto anatumia muda wake mwingi kuichambua ripoti hiyo kwa kuwa anataka awe Mwenyekiti wa Kamati ya PAC kinyemela.

Wakati huo huo huo Spika Ndugai aliwataka wabunge wawe wavumilivu kwa kutojadili mambo kabla muda wa kufanya hivyo haujafika kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Chanzo: Mtanzania
 
Kwahiyo CAG amewasilisha baadhi ya vitu visivyo vya kweli? Yaani watu wasijadili mambo hadi muda ufike? Ndiyo maana wabunge wengi wa ccm wanakuwa dhaifu sana katika kuchangia na kuchambua hoja kwakuwa wanatumia akili za kushikiwa
 
Mkuu unajua maana ya hoja kweli sio kila hoja ina ukweli mengine unaweza kuta hata aliyeleta hoja naye hajui alichokiingiza kama hoja na ndio maana hizo kamati zipo na hoja nyingine hufutwa baada ya kuoatiwa majibu
 
Supika ni ile tuliyoiona mtandaoni kupitia kwa CAG au na wewe umetengeneza yako?
Aweke yake tuichambue
Mbuzi kafia kisimani hahahhh
 
Spika wa Bunge Job Ndugai,amesema Mbunge wa Kigoma Mjini,Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) anawadanganya wananchi.

Ndugai alisema uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), unaofanywa na Zitto unalenga
kuwaaminisha wananchi kwamba kila kilichomo kwenye ripoti hiyo ni cha kweli.

Alisema kwa upande wake humuungi mkono kwa kuwa ukweli wa ripoti hiyo hudhihirishwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni kamati ya PAC na LAAC.

Spika Ndugai aliyasema hayo bungeni leo mchana muda mfupi kabla hajaahirisha Bunge hadi jioni.

Pamoja na hayo Spika alisema Zitto anatumia muda wake mwingi kuichambua ripoti hiyo kwa kuwa anataka awe Mwenyekiti wa Kamati ya PAC kinyemela.

Wakati huo huo huo Spika Ndugai aliwataka wabunge wawe wavumilivu kwa kutojadili mambo kabla muda wa kufanya hivyo haujafika kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Chanzo: Mtanzania
Ni kweli Zitto nadhani ana matatizo kwenye akili zake, ama kapungukiwa uwezo wa kufikiri au ni yale mazoea ya kupiga kelele ili apewe rushwa, yaani anajitahidi kutafuta mianya hata kama haipo anailazimisha ili wahusika waogope wampe rushwa, maana uchaguzi umekaribia na 2020 hatorudi bungeni hivyo anajaribu kutafuta namna ya kuishi baada ya kuondolewa bungeni 2020. Ni ukweli usiopingika kuwa ripoti ya CAG huwa ni maoni na huwa yanahitaji hatua nyingine na ndiyo maana ripoti hii huwezi kupeleka mahamakani ukawa ushahidi wa kumfunga mtu kwa sababu huwa wanasema hawana sufficient evidence ya kusema jambo hili au lile na hapo forensic au wale fraud examiner huwa wanaingia kazini. Nadhani Zitto angekuwa na akili timamu angesisitiza bunge liitishe hizo forensic au fraud examiner waingie kazini, lakini sasa unakuta kutumia upungufu wake wa uelewa ama akiwa anajua au makusudi au upungufu wa akili basi anaanzisha vitu halafu anavirusha kwenye mitandao na hivi watanzania wengi ni wavivu wa kujisomea basi wana download kama ilivyo nao wanaona pointi za kusemea na kusapoti bila kuchambua ukweli. Ila muda ni mwl mzuri sana, hakuna aliyewahi kumpinga Mungu akashinda. Mungu ibariki serikali ya awamu ya 5, Mungu Mbariki Mh. Ndugai na Bunge lake, Mungu Mbariki Dr Magufuli
 
Back
Top Bottom