Spika Ndugai mbona CUF na CCM waliwafukuza wanachama wake hukudai muhtasari wala Katiba, kwanini udai kwa CHADEMA?

YEHODAYA
Hebu nikuulize swali jepesi tu, kwani CCM na CUF ya Profesa Lipumba walipowafukuza wabunge wao, walifukuzwa na kikao cha Baraza Kuu??

Kama wao CCM na CUF ya Lipumba, waliwavua uanachama wabunge wao, kwa kupitia vikao vya CC vya vyama vyao, iweje Leo chama cha Chadema, kitumie njia hiyo hiyo, itokee Spika Ndugai anagomea maamuzi ya CC ya Chadema??

Hivi kwani Spika Ndugai hivi sasa amekuwa mhimili wa mahakama??
Weka katiba zao zinavyosema hapa kuhusu kufukuza mtu uanachama
 
Mtaweka thread nyingi wee za kuponda Ndugai weee hatoki mtu hadi baraza kuu Chadema muitishe litoe uamuzi

Hizi kelele zenu za kuanzisha thread kila dakika kuponda Ndugai wakati solution mnaijua ni kuitisha tu baraza kuu litoe maamuzi mnaonyesha mlivyojaa ujinga vichwani mwenu
Chadema iliwahi kumvua Zitto uanachama, mbona huyo supuka hakuomba katiba? Jibu ni eidha maelelezo ya shujaa wa afRiCa ama dunga ana intEreSt zake.
 
Hakika inashangaza na kustajabisha kwanini spika aliyeapa kuulinda na kuitumikia katiba ya nchi leo ndio anakuwa kiongozi tena wa mhimili anaivunja Katiba kwa makusudi na kuteteta uvunjaji wake wa Katiba na Serikali kupitia Mwanasheria mkuu wa Serikali ipo kimya.

Spika huyo huyo aliwahi kuwafukuza wabunge 8 wa cuf baada ya mwenyekiti wa CUF Prof.Lipumba kumwandikia barua Spika Ndugai ya kumtaarifa juu ya kufukuzwa kwao na kuwaapisha wengine haraka na Spika Ndugai hakudai muhtasari wala katiba ya CUF. Kama haitoshi Spika Ndugai huyo huyo aliwahi kumfukuza mbunge Sophia Simba baada ya chama chake cha CCM kumfukuza uanachama na hatukumsikia Spika Ndugai kudai muhtasari wala Katiba ya CCM je kwanini CHADEMA ndio wanatakiwa kupeleka muhtasari

Na katiba ya chama?

Ni wazi suala hili spika ndugai inawezekana ana maslahi binafsi na hao wabunge fake 19 na ukimya wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tume ya uchaguzi kutokujibu barua ya CHADEMA kwa miezi 5 sasa na pia kitendo cha DPP kumtoa mmoja wa hao wabunge mahabusu ili akaapishwa vitendo vyote hivyo vinaashiria ni mpango uliopangwa.
Huyu ana ugonjwa kama mwendazake.
Iko siku atajuta
 
Tatizo ni pesa kutoka jumuiya ya madola, wasipokuwepo wabunge wa upinzani kuongoza baadhi ya kamati hizo pesa hawatapewa. kipindi hicho kulikuwa hakuna hilo hitaji.
 
MATONYA MWEREVU SANA.CCM MNATUKOSEA SANA KUPITIA SPIKA/NAIBU WAKE.
Kuleni kichwa , wacheni maneno mengi, spika wa aina hii anaitia aibu Nchi,
Upinzani Tanzania unahitaji kuheshimika, Bila ya kuondoka na kichwa cha mtfedhuli itabaki story tuu.
 
Hiyo ni mipango waliyoipanga tangu uchaguzi wa serikali za mitaa 2019,uchaguzi mkuu 28 Otober 2020 waliostahili wasiwepo bungeni kwa mujibu wa sheria wameingizwa kimabavu kwa sababu ya rushwa ya ngono.
Basi ngono kwa hao mothers ni tamu sana..kama viongozi wanatoa kafara m.12*19 per month kisa ngono..huo utamu si huu ninaoujua mm.
 
Chadema inajindhhoofisha yenyewe kwa nini msiite mkutano wa baraza kuu kama katiba inavyosema mumalize hilo tatizo?
Kikao cha Baraza kuu hakiitishwi kwa matakwa ya mjinga mmoja anayesigina katiba ya nchi, bali kwa kufuata katiba ya chama.

Ndugai anaonekana mjinga kuhangaika na mchakato wa kuwafukuza uanachama covid 19, wakati siyo hoja ya msingi.

Hoja ya msingi ni kuwa CHADEMA haijawahi kuteua wabunge wa viti maalum. Yeye aliletewa na nani majina ya hao covid 19?

Ndugai, kwa ujinga anaoufurahia, anataka kuwaaminisha wajinga wenzake kuwa CHADEMA ilikuwa na wabunge, na sasa CHADEMA emewafukuza uanachama.
 
hoja ya msingi ni kuwa CHADEMA haijawahi kuteua wabunge wa viti maalum. Yeye aliletewa na nani majina ya hao covid 19?
Waulizeni hao wabunge wenu kwenye kikao cha Baraza KUU Wako tayari kuwaelezeni huko mbona mnakuwa wazito kwa hilo? wakati wao wako tayari kuwaambia kila kitu,Mnakwepa nini? wabunge wenu wapo na wana utayari ninyi mnagomea nini?
 
Bahati mbaya tuna spika ambaye hana chembe ya hekima wala uadilifu.

Kabla covid 19 hawajaapishwa, CHADEMA walitamka kuwa hawajawahi kufanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum. Ni nini kilichomkimbiza huyu spika mnafiki kwenda kuwaapisha kwenye garage? Kwa nini baada ya kusikia tamko la CHADEMA kutofanya uteuzi, spika asingechukua muda kujitidhisha, na badala yake akakimbilia kuwaapisha?

Wala tusizungushe maneno, tuna spika wakala wa shetani, anayeuabudu uovu.

Kwa ushauri wangu CHADEMA isipoteze muda kufanya hayo anayoyataka huyu muovu. CHADEMA walitimiza wajibu wao wa kumjulisha spika kuwa hawajafanya uteuzi, inatosha. Huyu muovu akae na hao wabunge wake, kama si leo au kesho, huyu spika muovu ataulipia uovu wake.

CHADEMA, wazidi kuweka wazi nyaraka zote zinazoonesha jinsi walivyotimiza wajibu wa kisheria na kikanuni. Wasipoteze muda kubishana na mtu mwenye dhamira ovu. Tumwache Ndugai aendelee kuishi katika uovu, na malipo yake, bila shaka hayatakosekana.
 
Bado kidogo ataomba muhtasari uliompitisha Rais Samia awe Mkuu wa Nchi.

Akili yake ni sawa na wapiga meza bungeni.Nape jiuzulu
 
Ndugai bado ana kile kiburi alichopandikiziwa na Magufuli na kupewa kinga feki. Nchi hii nasema haijawahi kupata spika mpumbavu kama huyu.
 
SUKUMA na TAGA wewe.
Babu yako Magufuli alijifanya lkn kaiacha chadema ipo hai.

Lakini kaisambaratisha,, nyalandu nae kawakimbia. Hicho chama kiendeshwe na msukuma, mtu wa pwani, kanda ya kusini ama magharibi utaona kama hakijapata wanachama.
 
Angalia kichwani kwake ndio utajua sababu

Screenshot_20210423-185800.png
 
Mleta mada swali katiba zao ziko sawa na ya Chadema kuhusu wanachama kufukuzwa uanachama? Ya CHADEMA INATAMKA WAZI KUWA Baraza kuu ndio final zao zinasema hivyo?

Pili Unajua kuwa waliambatanisha au la kwani wewe ulikuwa Spika uliyepokea hizo barua?

Mnakwepa kwepa tuu itisheni baraza kuu litoe maamuzi kama katiba yenu inavyosema.Mnataka serikali isimamie katiba ya nchi ninyi ya kwenu tu Chadema inawashinda.Itisheni mkutano wenu wa baraza kuu mumalize hilo jambo mnajaza server za jamii forums bure

Chadema chama cha hovyo sana .
Suala sio kufanana kwa Katiba suala ni Viambatanisho Tumia Akili ya Binadamu acha kutumia za mbwa
 
Binafsi Nina wasiwasi Sana na ndugai kwenye swala hili la wabunge 19 au covid-19.Huenda Kuna rushwa ya kingono au rushwa ya pesa, Sio bure
 
Back
Top Bottom