Spika Ndugai: Makonda ni Mtani wangu, hivyo msijali maneno yake

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,055
Bila shaka hili ni dongo zuri kwa Makonda, na ni sawa na kusema watu wayapuuze maneno anayoyaongea kwa kuwa ni utani tu

Siku moja baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutakiwa kutimiza ahadi yake ya kuweka vifaa vya kupima wabunge kama wametumia kilevi ama dawa za kulevya kabla ya kuingia Ukumbi wa Bunge, amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni mtani wake, hivyo watu wasijali maneno yake. Aidha, katika Mkutano wake uliofanyika juzi, Makonda alimuomba Spika Ndugai kuweka kipimo hicho ili kabla wabunge hawajasimama kuchangia hoja wabainike kama wanatumia dawa za kulevya au la.

Chanzo: Dar24
 
ndugai ameamua kummdharau !!!! ametumia akili sana......
kaona ni upuuz kumpa kiki, yaani waache kufanya mambo ya msingi wahangaike na mkurupukaji huyu, kulumbana kila siku na wenziwe... hana kaz?!i huko buguruni wakazi wa maeneo hayo wanalalamikia kero ya matakataka na sehemu yenyewe si mbali sana kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa badala ahangaike na kero za wananchi wake anahangaika na mambo ya bungeni
big up ndugai
 
Kapangua hoja kiutu uzima tayari ya kupimwa wabunge kabla ya kuingia bungeni kuona kama wanakula unga.

Ila azma ya kumuwajibisha iko pale pale.

Namuona Ndungai kama mmoja wa wanaoweza kuchukua fomu ya Oifsi kubwa, pindi Mukulu akimaliza muda wake.
 
Hivi bunge nalo lipo Dsm au kuhamia Dodoma hadi mamlaka ya mkuu wa mkoa wa DSM nayo yanaamia Dodoma. Huu muhimili kweli una mizizi mirefu. Hadi watumishi wa muhimili huu wanakuwa na sauti dhidi ya mihimili mingine yote.
Well bro Konda ebu mrushie taulo yule nabii anayesota Kisongo kwa ndoto za maono (najua kwa kufanya hivyo utakuwa umedhihirisha mauwezo yako zaidi)
 
"......I've always found it easier to be funny than to be serious...."

Molly Ivins
 
Hii nchi ina matatizo yanayozidi akili za wenye nayo.

Hadi rais naye anatania kwenye mambo nyeti kama uzazi wa mpango.

Nadhani huu utawala wote kwa ujumla ni utani na usanii ndio maana kila wiki lazima watuwekee filamu ya kutazama.
 
Hivyo ndivyo watu wenye busara umaliza tofauti zao, sio kama mh. Lema, matokeo yake unaishia "shimoni"
 
Wabunge wanachukulia mambo serious kuwa utani.

Swala la kuwapima wabunge ni jambo serious
Lupyee
Bunge huongozwa kwa kanuni...sio kila anachosema mtu kinakuwa kanuni za bunge...PM aombe kanuni zifanyiwe mabadiriko na hicho kipengele kiongezwe.
Hana mamlaka hata kidogo ya "Kumwamru spika"
 
Wapimwe tu tunahofu wauza ngada wanasniff halafu wanakaa ktk bunge na kuporoja tu bila fact.
Foristance mzee wa shanga
 
Bila shaka hili ni dongo zuri kwa Makonda, na ni sawa na kusema watu wayapuuze maneno anayoyaongea kwa kuwa ni utani tu

Siku moja baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutakiwa kutimiza ahadi yake ya kuweka vifaa vya kupima wabunge kama wametumia kilevi ama dawa za kulevya kabla ya kuingia Ukumbi wa Bunge, amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni mtani wake, hivyo watu wasijali maneno yake. Aidha, katika Mkutano wake uliofanyika juzi, Makonda alimuomba Spika Ndugai kuweka kipimo hicho ili kabla wabunge hawajasimama kuchangia hoja wabainike kama wanatumia dawa za kulevya au la.

Chanzo: Dar24
kamjibu kinyume akijuwa kijana wanaenda ku mphase out mpaka hatoamini. asante mkubwa NDUGAI.
 
Back
Top Bottom