Spika Ndugai: Kwenye majadiliano ya mikataba ya kimataifa tusipeleke watu waliopata makarai "O" level "A" level na Chuo kikuu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,613
141,436
Spika wa bunge mh Job Ndugai ameitaka serikali kuwa makini inapounda timu za kufanya majadiliano ya kimataifa ( negotiations) na kupeleka watu makini badala ya wababaishaji.

Serikali isiangalie tu kuwa huyu ni Mkurugenzi, RC au Katibu bali iangalie sifa zake alipokuwa shule.....peleka watu waliopata division 1 O level na A level kisha first class degree chuo kikuu hata kama ni vijana wadogo amesisitiza Ndugai.

Haijalishi ukurugenzi umeupataje cha msingi ni je una vyeti vinavyoheshimika, amemalizia Spika Ndugai.

Spika Ndugai ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Mmmh???? Prof. nao wapo kwenye hili kundi? Mbona wanaharibugi hivyo? Ni mtazamo tu
 
Etii??? amesahau ya kwamba siku hizi kuna degree na first class nyingi tu za chupi, wasomi wengi huko wanajua kukariri lakni kwenye kupambanua mambo ya msingi ni weupe yaani unaona bora hata raia wa kawaida wa mtaani wanaweza jenga hoja na kutetea hoja tofouti na hao wanoitwa vipanga wa chuo kikuu.
 
Elimu ya darasani kukariri ni tofauti na maarifa.Mbuge wa Kahama Mh. Kishimba namkubali sana kwa hoja zake japo huenda hakumaliza hata elimu ya Msingi., anawazidi maprofesa na Madoctor wengi.
 
Sio kila mwenye 1st Class ana skills ya negotiation,

Negotiations ni Taaluma pia ni Kipaji

Kwa mfano mh. Charles Mwijage hakuwa na 1st class lakin ni negotiator Mzuri sana

Labda isemwe negotiation course ziwe compulsory baadhi ya Watumishi wa Umma ambao wana 1st class kwenye Shahada zao

Sio kila Straker mzuri lazima awe Kocha mzuri
 
Back
Top Bottom