Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Inasikitisha kumuona Spika wa Bunge linaloitwa la " Bunge la Jamhuri ya Muungano" kuonekana kusononeka na kuudhika ndani ya nafsi pale mbunge kutoka Zanzibar atakapotoa hoja ima kutaka ufafanuzi au kuhoji shauri lolote kuhusu taasisi za Muungano hususan mustakabali na maslahi ya Zanzibar.
Mfano hai mikononi, ni leo asubuhi wakati wa kipindi cha maswali na majibu,Mbunge chipukizi Ali Salim wa Mwanakwerekwe Zanzibar akitakakujua Mmiliki wa ATCL, Shirika la Ndege na malimbikizo ya deni ya "Landing charges" liliofanywa na shirika hilo viwanja vya ndege vya Zanzibar.
Swali lilikuwa jepesi na rahisi. Naibu waziri wa Ujenzi alijibu kuwa Mmiliki wa ATCL ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na inamiliki hisa kwa 100% na kuwa kuhusu madai ya " Landing charges" amepewa CAG " kuyahakiki" .
Ndipo Mhe. Ali Salim alitaka kujua kuwa kwa vile mmiliki ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hisa za Zanzibar katika shirika hilo ni asilimia ngapi?
Alizidi kufafanua kuwa hata BoT inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano lakini bado Zanzibar ina hisa ya 12%
Ilionekana jibu lilimkwama kidogo Naibu Waziri lakini ilikuwa rahisi kwa mhe. Spika kumrushia "maneno" ya kuonesha rangi zake asili na jinsi alivyoudhika na swali hilo la nyongeza
Hivi kazi ya mbunge kutoka Zanzibar kwenye bunge la Jamhuri la muungano ni nini hasa? kupiga makofi na kusema " ndiooooo". Kazi y mbunge ni kuja kutetea maslahi ya Zanzibar? Je ni kosa kutetea haki na kuonesha wapi Zanzibar wanapo dhulumiwa haki yao?