GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,548
- 108,860
Siku hizi unaongozwa sana na:
1.Majungu
2.Uswahili
3.Mihemko
4.Unafiki
5.Visasi
6.Chuki
7.Sifa
Ninavyojua ni kwamba Spika wa Bunge huwa hana tofauti na Mwamuzi ( Referee ) ambapo hutakiwa sana kuwa ‘ neutral ‘ japo anaweza kweli akawa na Mahaba / Mapenzi upande fulani ila mwenzetu Wewe umeshindwa kabisa kuwa Referee bora wa mechi ya Derby baina ya Wabunge wa CCM na wa UPINZANI.
Kauli zako ulizozitoa jana wakati wa upigwaji Kura ili kupitishwa kwa Bajeti sidhani kama kweli zilitakiwa zitolewe na Spika wa Bunge bali kama ningezisikia kutoka kwa Msukuma au Sugu wala nisingezishangaa sana kwani wanajulikana na tumewazoea.
Ombi langu Kwako Mheshimiwa Spika naomba katika Vikao vijavyo nimuone Yule Job Ndugai mwenyewe wa miaka saba ( 7 ) iliyopita ambapo alikuwa ni Mtu makini, mkweli na muwazi kwa pande zote mbili zilizopo ndani ya Bunge vinginevyo nisikufiche kwa haya unayoyafanya sasa ‘ credibility ‘ yako inashuka kwa kiwango kikubwa na kwa kasi kubwa mno.
Nawasilisha.