Spika Ndugai jirekebishe haraka kwani kila siku Credibility yako inashuka tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,583
2,000
Siku hizi unaongozwa sana na:

1.Majungu

2.Uswahili

3.Mihemko

4.Unafiki

5.Visasi

6.Chuki

7.Sifa

Ninavyojua ni kwamba Spika wa Bunge huwa hana tofauti na Mwamuzi ( Referee ) ambapo hutakiwa sana kuwa ‘ neutral ‘ japo anaweza kweli akawa na Mahaba / Mapenzi upande fulani ila mwenzetu Wewe umeshindwa kabisa kuwa Referee bora wa mechi ya Derby baina ya Wabunge wa CCM na wa UPINZANI.

Kauli zako ulizozitoa jana wakati wa upigwaji Kura ili kupitishwa kwa Bajeti sidhani kama kweli zilitakiwa zitolewe na Spika wa Bunge bali kama ningezisikia kutoka kwa Msukuma au Sugu wala nisingezishangaa sana kwani wanajulikana na tumewazoea.

Ombi langu Kwako Mheshimiwa Spika naomba katika Vikao vijavyo nimuone Yule Job Ndugai mwenyewe wa miaka saba ( 7 ) iliyopita ambapo alikuwa ni Mtu makini, mkweli na muwazi kwa pande zote mbili zilizopo ndani ya Bunge vinginevyo nisikufiche kwa haya unayoyafanya sasa ‘ credibility ‘ yako inashuka kwa kiwango kikubwa na kwa kasi kubwa mno.

Nawasilisha.

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
14,356
2,000
Bunge hili lina bahati mbaya kuongozwa na wasomi wawili wenye mihemuko, jazba, majivuno na maelekezo ya party caucus. Kwa kweli sijui afadhali ya nani kati ya Ndugai na Tulia?!
 
Mkomavu

JF-Expert Member
Jan 25, 2016
11,103
2,000
Yule mtu aliumwa sana pengine ugonjwa ulipitia sehemu za ufahamu na kumfanya awe vile tumuombee busara,hekima na upendo
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,281
2,000
Siku hizi unaongozwa sana na:

1.Majungu

2.Uswahili

3.Mihemko

4.Unafiki

5.Visasi

6.Chuki

7.Sifa

Ninavyojua ni kwamba Spika wa Bunge huwa hana tofauti na Mwamuzi ( Referee ) ambapo hutakiwa sana kuwa ‘ neutral ‘ japo anaweza kweli akawa na Mahaba / Mapenzi upande fulani ila mwenzetu Wewe umeshindwa kabisa kuwa Referee bora wa mechi ya Derby baina ya Wabunge wa CCM na wa UPINZANI.

Kauli zako ulizozitoa jana wakati wa upigwaji Kura ili kupitishwa kwa Bajeti sidhani kama kweli zilitakiwa zitolewe na Spika wa Bunge bali kama ningezisikia kutoka kwa Msukuma au Sugu wala nisingezishangaa sana kwani wanajulikana na tumewazoea.

Ombi langu Kwako Mheshimiwa Spika naomba katika Vikao vijavyo nimuone Yule Job Ndugai mwenyewe wa miaka saba ( 7 ) iliyopita ambapo alikuwa ni Mtu makini, mkweli na muwazi kwa pande zote mbili zilizopo ndani ya Bunge vinginevyo nisikufiche kwa haya unayoyafanya sasa ‘ credibility ‘ yako inashuka kwa kiwango kikubwa na kwa kasi kubwa mno.

Nawasilisha.

Ndugai hana kosa, siku ya repoti ya Makinia alipewa maagizo na mwenyekiti wa chama pale ikulu, Watanzania wote mkaa kimya na kulewa makinikia, sasa Ndugai anatekeleza maagizo ya Boss wote kimya tuache unafki.

Kama hatupendi ubabaishaji kwenye nchi Bwana mkubwa aambiwe waziwazi kwamba anasigina katiba na siyo kumfanyia maandamano ya kumpongeza fundi makenika uliyempelekea gari yako atengeze sasa limepona ati unaandamana kumpongeza, jema lifanywalo na Rais ni wajibu wake kikatiba na ni yeye binafsi aliomba kazi hiyo.
 
Negongo

Senior Member
Apr 2, 2012
102
225
Kwa kweli hata mie nakuunga mkono, namchukia sana siku, kila siku ni kuwaonea tu wapinzani, anataka aogopwe kama mungu, anadhani bunge ni shule ya msingi.
 
Msarendo

JF-Expert Member
Jan 29, 2011
9,905
2,000
hajawai kuwa fair huyo ndugai, kipindi kile anaumwa alipata akili kidogo, sasa amepona karudia tabia yake ya dharau
 
chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,678
2,000
Change na mapungufu yake tote lakini anajua kulimudu bunge

Zungu naye amri zimekuwa nyingi kama jeshini
 
kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
2,379
2,000
Kuna mdau aliandika eti ugonjwa wake anougua ni wa kufumuka hasira,huyo mdau mkuu!!
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,107
2,000
Nakubaliana na mtoa mada,ni kweli pamoja na SPIKA kuwa umetokea kwenye chama na somehow utakuwa na mapenzi na chama chako,ila unapokaa kwenye kile kiti ni vema ukaonyesha na kutekeleza majukumu yake sio kuwa ni rungu la serikali kuuwa oppositions,yes inaelekea hii nchi yetu inasukumwa kwenye mfumo wa chama kimoja,na madhara yake wote tunayaelewa,hata katika maisha yetu ya kawaida kama hujishindanishi kimaendeleo end of the day utakuwa husogei,upinzani ni kioo cha kujiangalia na kujishindanisha,angalia mifano ya US vs CHINA,clubs za mipira,nokia vs Samsung etc etc
 
Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,080
2,000
Naunga mkono hoja!
Hana tofauti na wanawake wa pwani vijembe vingi mpaka anakera
 
edicom

Member
Oct 4, 2011
11
45
Mfano tu Jana yule mbunge Mwita Waitara alitolewa nje kwa uonevu tu binafsi mi sikuona kosa alilofanya
 
lauzi96

JF-Expert Member
Jul 10, 2014
423
1,000
jana hakueleweka kama ni spika au mbunge
maana naye alikuwa anachangia pia hakuwa referee mzuri kajishushia heshima aliyojitengenezea miaka mingi
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,520
2,000
bunge limepoteza hadhi yake yaani kuna ubaguzi wa wazi kati ya ccm na upinzani. nchi ikifikia hapo ni hatari
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom