Spika Ndugai: Hotuba za upinzani huwa zinaandaliwa mitaani na mawaziri vivuli huzisaini tu bila kuzipitia

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,894
141,827
Spika wa bunge mh Ndugai amesema Hotuba za kambi ya upinzani huwa zinaandaliwa mahali fulani huko nje ya bunge na mawaziri vivuli huzisaini tu bila kuzihakiki. Hivyo ili kulinda heshima ya bunge na kuhakikisha kama kanuni zimezingatiwa ni lazima zihakikiwe.

Spika amesema kuna mambo yako mahakamani hivyo yakiingizwa kwenye Hotuba yanaweza kuleta migongano kwa mihimili hii miwili yaani bunge na mahakama na yeye hawezi kuruhusu hali hiyo itokee.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom