Spika Ndugai hana mamlaka ya kupinga maamuzi halali yaliyofanywa na Kamati kuu ya CHADEMA

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Nimeshangazwa sana na kauli aliyotoa Spika Ndugai hivi leo, wakati akiwaapisha wabunge wapya Humphrey Polepole na yule mwanamama Riziki Lulida, kuwa wabunge wa kuteuliwa na Rais katika zile nafasi zake 10 alizopewa kwa mujibu wa Katiba

Spika Ndugai amenukuliwa akisema kuwa hatambui maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu ya Chadema na akaendelea kusisitiza kuwa ataendelea kuwatambua wabunge hao 19 aliowaapisha wiki iliyopita kuwa ni wabunge halali!

Nimkumbushe tu Spika Ndugai kuwa yeye analazimika kuongoza Bunge lake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977

Katiba hiyo katika ibara ya 71(1)(e) inasema kama ifuatavyo nanukuu:-

Ibara ya 71(1)
Mbunge yeyote atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake litokeapo lolote kati ya yafuatayo.

Ibara ya 71(e)
Ikiwa Mbunge huyo atakoma kuwa mwanachama wa chama cha siasa alichokuwemo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge.

Katiba ya nchi yetu haina wagombea binafsi, sasa tumuulize Spika Ndugai anaposema kuwa ataendelea kuwatambua wabunge hao waliuvuliwa uanachama wao na Chadema, atawatambua wakiwa ni wanachama wa chama gani?

Sasa sielewi Spika Ndugai anaposema kuwa hao wabunge wa viti maalum wa Chadema wataendelea kuwa wabunge, anasimama katika Ibara ipi katika Katiba hii ya nchi?

Wenyewe tumeisoma Katiba ya nchi na ipo wazi sana katika suala hili.

Nimkumbushe tu Spika Ndugai kuwa hii siyo Mara ya kwanza kwa chama cha siasa kufukuza wanachama wake na Bunge hilo likatii maamuzi hayo ya Chama, kwa kuwa ndivyo inavyotakiwa kwa mujibu wa Katiba.

Mwezi March 2012, Chama Cha Mapinduzi kiliwafukuza wanachama wake 12 na miongoni mwao alikuwemo, Sofia Simba, aliyekuwa Mwenyekiti wa wanawake, ambaye pia alikuwa ni mbunge.

Kilichofuata ni huyo Sophia Simba kuvuliwa ubunge wake, kwa kuwa lilikuwa ni sharti la Kikatiba.

Mwezi July 2017, Kikao cha Kamati Kuu cha CUF kiliwavua uanachama wao wabunge wanane wa chama hicho.

Vile vile Bunge hilo lilitekeleza Mara moja na kuwavua wabunge hao, ubunge wao kwa kuwa ni kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Sasa swali linakija ni kwanini chama cha Chadema kilivyotekeleza sharti hilo la Kikatiba, Bunge hilo hilo liwe na maamuzi tofauti?

Hii double Standard ya utekelezaji wa sheria inatokana na nini?

Nimalizie kwa kusema kuwa Spika Ndugai hana mamlaka yoyote ya kikatiba ya kuingilia maamuzi yaliyofanywa na chama cha kisiasa kinachotambulika kihalali na msajili wa vyama vya siasa.

Anachofanya Ndugai ni kuiingiza nchi hii katika mgogoro mkubwa wa Kikatiba ambao haujawahi kutokea katika siku za nyuma.

Kwa maana hiyo watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunapaswa kumkemea kwa nguvu zetu zote huyu Spika Ndugai, kwamba anaipeleka nchi hii na kuitumbukiza shimoni
 
Tatizo siyo Ndugai.Tatizo limejificha hapa
87659087.jpg
 
Awamu hii hawafuati sheria za nchi, usijisumbue, wanajua vizuri kabisa wanavunja sheria lakini hawajali, msijichoshe kupigia mbuzi gitaa, muhimu tuombe kama taifa siku ziende haraka mwisho wao ufike waondoke, au Mungu akipendezwa awapende zaidi mapema.
 
Nimeshangazwa sana na kauli aliyotoa Spika Ndugai hivi leo, wakati akiwaapisha wabunge wapya Humphrey Polepole na yule mwanamama Lulida, kuwa wabunge wa kuteuliwa na Rais katika zile nafasi zake 10 alizopewa kwa mujibu wa Katiba...
Tatizo la ndugai,kwa sababu ya nafasi aliyopo anadhani kuwa yeye pekee yake ndo msomi saaaana hapa Tz.anadhani yeye ndo kila kitu.
Nimeshangazwa sana na kauli aliyotoa Spika Ndugai hivi leo, wakati akiwaapisha wabunge wapya Humphrey Polepole na yule mwanamama Lulida, kuwa wabunge wa kuteuliwa na Rais katika zile nafasi zake 10 alizopewa kwa mujibu wa Katiba...
Kauli na msimamo ya ndugai uko sawa kama nchi hii hatuzingatii utawala wa kikatiba,Lenakini kama tuna katiba kama nchi huru ,ndugai you are wrong.
 
Tatizo siyo Ndugai.Tatizo limejificha hapaView attachment 1638616
2017, CCM ilimfukuza Sophia Simba (akiwa mwenyekiti wa UWT na mbunge wa VM) kwa tuhuma zikiwepo kumuunga mkono Edward Lowassa (aliyehamia CCM wakati huo). Lakini Ndugai hakusimama kusema CCM hii ya Magufuli inawanyanyasa wanawake. Ikawasamehe wanaume na kumpa adhabu mwanamke.
 
Back
Top Bottom