Spika Ndugai, hamkuona uvuvi wa bahari kuu unaweza kulipatia taifa mapato kuliko kuwakakamua wananchi?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,513
2,000
Nimeshangazwa sana na kauli ya spika wa bunge la JMT kupigia chapuo tozo za miamala ya simu kwa madai kuwa eti ni muhimu kwa maendeleo ya jimbo la Kongwa na taifa letu.

Mbaya zaidi anadai eti hana uhakika kama kuna vyanzo vingine vya mapato zaidi ya kuwakamua wananchi kupitia tozo za miamala ya simu. Huku ni kujitoa fahamu na kutokubali makosa.

Hivi ni meli ngapi za nje zinavua na kuacha kulipa mapato kwenye eneo letu la bahari kuu? Kama serikali ingeweka mkazo ili hizi meli zilipe kodi, je kulikuwa na haja ya kuwakamua wananchi wa kawaida?

Ndio kusema Ndugai na Bunge lako lote mlikaa na kuumiza kichwa na kuona eneo pekee kama chanzo cha kodi ni kuwakamua wanachi?

My take: 2025 sio mbali, wananchi wasifanye makosa.
 

Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,716
2,000
Kutishia 2025 nakupa pole.

1. Ndugai anaharibu kwa kuwa ni mstaafu mtarajiwa.(hana cha kupoteza)
2. TZ uchaguzi huwa nikumtangaza mtu wanayemtaka na kumnunua yeyote
3. Ndugai analazimisha tozo ili mafao yake ya Usipika isiwe shida.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom