Spika Ndugai: Hakuna Mbunge aliyefukuzwa Ubunge. Vikao vya majungu havifanyi kazi hapa, Msajili tazama vyama vya namna hii

Baada ya Kamati Kuu ya CHADEMA kukaa na kuamua kuwafukuza uanachama Wabunge wanne waliokiuka taratibu za chama hicho kwa kuhudhuria vikao vya Bunge tofauti na kilivyoamua Spika Ndugai awataka waliofukuzwa kutokuwa na hofu

Spika Ndugai amesema "Wabunge mnaapishwa na Spika na karibia wote humu nimewaapisha mimi mwenyewe sasa Wabunge niliowaapisha wala msiwe na wasiwasi hakuna cha nini wala nini vikao vya majungu hivyo havifanyi kazi"

Amesema, "Eti mmoja katika nchi hii anajifanya yeye ana mamlaka ya kufukuza Wabunge anavyotaka. Hivi nani jina lake huyo? Hii haiwezekani bwana. Haiwezekani hiyo biashara itaishia huko huko ila sio Tanzania. Tanzania hapa huwezi kujenga ufalme wa namna hiyo”

Ameongeza, “Yaani unafanya unavyotaka, Wabunge kushoto, kulia geuka sawa. Haya inama, nyanyuka. Mbunge ukipata mshahara lete sehemu fulani ya mshahara, lete huku. Wananchi mnachagua Mbunge halafu awe mtumwa wa mtu? Kweli? Akihudhuria kikao cha Bunge adhabu yake ni kufukuzwa? Hila jambo halipo”

Amesisitiza "Wale mnaoendelea kuhudhuria endeleni tutawalinda wala msiwe na mashaka kwa sababu hakuna jambo lolote mmefanya kinyume na sheria halipo kabisa. Na msajili tazama vyama vya namna hii”

Aidha amemalizia kwa kusema “Sijui kwa kuwa yeye mwenyewe anaona Novemba harudi hapa sasa anawaharibia wenzake. Mambo magumu haya ila sio magumu kihivyo
Kumbe katiba ni takataka tu
 
Sasa Ndugai si utumie akili kidogo tu, hao wamefukuzwa uanachama. chama hakiwatambui kama wanachama na wabunge kutoka CHADEMA.

Sasa wewe ukiamua kuwakumbatia nani amekukataza. Mbona unaingilia sana maamuzi ya chama kisichokuhusu. Shida yako nini?

Kufukuzwa uanachama mbona siyo big deal kihivyo.
Wewe unawaapisha wabunge, ni sawa lakini wanafikaje hapo bungeni? Wanaingia kwa tiketi yako? Yaani wewe ndiye mdhamini wao?

Unatoka mishipa bure kwa jambo lisilokuhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
ni kama spika hajui thamani yake na ukubwa na unyeti wa taasisi anayoiongoza
 
Kuna hoja ya msingi, wabunge wanachaguliwa na wananchi, hivyo kubadili itikadi isiwe sababu ya kubeza wananchi. Katiba ifanyiwe marekebisho ku-accomodate hiyo haki ya msingi ya mtu kuamua chama akitakacho wakati wowote bila ya hofu ya kupoteza ubunge. Issue ya spika is out of proportion i dont have energy to ponder
Kama katiba inabadilishwa kipambavu hivi bora na utawala wa kifalme ieleweke. Yaani mkibanwa huku mnabadilisha pale mkibadilisha pale mkaona mnabanwa mnabadilisha huku. Yaani vuluvulu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa Mbowe wakati mwingine maamuzi yake yanakuwa ya kupaniki sana, ndio maana watu tunataka Katiba mpya itakayoondoka na udikteta wa vyama kama huu.

Mbunge hata kuhojiwa hajahojiwa unamtimua hakuna hata kumpa onyo la kwanza ama la pili

Tunaupinga udikteta wa Magufuli huku tukiuishi huohuo udikteta tunaoupinga.

Ilipaswa waitwe wahojiwe kabla ya kuchukuliwa hatua ya jumla kama hii.
Onyo la nini ,walishaongea kwa pamoja wasiende bungeni ,wao wakaenda na kuanza kuwakejeli wengine ,kuwa kinyume na maamuzi ya wengi ni usaliti ndo maana wakafukuzwa
 
Anavyosema eti Mbowe hatorudi bungeni yeye anauhakika gani kama anarudi?. Mara hii kasahau kuwa watanzania woote tunaelewa gonjwa sugu linalomsumbua yeye na baadhi ya wabunge kama Mr. Mkono na kwamba gonjwa lenyewe halina dawa . Tayari maji marefu chali aache kumdhihaki Mungu
Mkuu kumbe unajua na wewe mzee anaumwa nini?? Daaah hatar fayaaa yale mambo ndiyo yalivo

Sent by IPhone
 
Mkuu usipaniki unapasw kufikiri kwa kina kabla ya kuunga kila kitu ilimradi kimefanywa kamati kuu.
Hivi unaelewa wewe
Wamefukuzwa uanachama sio ubunge Acha ujinga wewe

Sent by IPhone
 
Kweli kabisa Mbowe wakati mwingine maamuzi yake yanakuwa ya kupaniki sana, ndio maana watu tunataka Katiba mpya itakayoondoka na udikteta wa vyama kama huu.

Mbunge hata kuhojiwa hajahojiwa unamtimua hakuna hata kumpa onyo la kwanza ama la pili

Tunaupinga udikteta wa Magufuli huku tukiuishi huohuo udikteta tunaoupinga.

Ilipaswa waitwe wahojiwe kabla ya kuchukuliwa hatua ya jumla kama hii.
wewe unajua sana kuliko kamati kuu iliyotoa uamuzi?
 
Inanikumbusha kitu kimoja Mkururgenzi wa Ubungo alipopokea barua feki fasta tu akatolea maamuzi ya kutomtambua Meya..hapa Cahadema wamefanya maamuzi halali Sabufa anasema hayatambui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugai anavunja katiba, kama anaona hali Ni mbaya amshauri waziri wa sheria wapeleke marekebisho ya katiba ili kuruhusu mbunge akifukuzwa Na chama chake asiondolewe ubunge. Hii Tabia ya spika kuvunja katiba haikubaliki kamwe.
Hao wabunge wapewe nafasi ya kusikilizwa au kuwepo na chombo cha kukata rufaa, hili swala la mtu mmoja akiamua ameamua si vyema hata kidogo

wapeleke mswaada bungeni , viundwe vyombo vitakavyo shughulikia maswala kama haya, imagine miaka yako yooote mitano inaenda potea hivi hivi Kwasababu ndogo ndogo ambazo mnaweza ongea mkayamaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom