Spika Ndugai, hadi lini unajibanza kwenye uongo, ulaghai, utapeli na kutumika? Hufanani na uyafanyayo. Umepatwa na nini?

Kuongoza ni kuweka ukweli mbele. Ni kukumbatia na 'kushare' haki kwa unaowaongoza. Ni kufuata taratibu zilizopo huku ukitanguliza maslahi ya unaowaongoza, haki zao na wajibu wao. Kuongoza si kujitutumua, kujianika na kujichora kuwa una nguvu au una uwezo wa kuamua utakavyo. Uongozi si rafiki wa uongo, ulaghai na utapeli.

Spika Job Yustino Ndugai, umepotoka. Umejibanza kwenye uongo, utapeli, ulaghai na ni Dhahiri kuwa unatumika. Ninalazimika kuongea kwa uchungu na ukali kwako kada mwenzangu na kiongozi wangu wa CCM (najua unaingia Kamati Kuu ya CCM na mikutano mingineyo kwa nafasi yako). Amini nakwambia, ulikojibanza si sehemu salama wala hakutakusaidia.

Umekuwa ukiwatimua Bungeni Wabunge mbalimbali wa Upinzani ukisukumwa na hisia na kutaka kwako kuonekana kuwa wewe ni mtumishi muaminifu wa CCM na unayafanya yenye baraka za CCM. Katika hilo, umekuwa kila mtanzania ajue kuwa unawashughulikia wapinzani ndani ya Bunge(inadaiwa unatekeleza agizo la Mwenyekiti wetu alilolitoa Ikulu). Wapinzani wamekuwa wakikosa fursa ya kujitetea, kupata nafasi ya kufurukuta na kadhalika.

Kuhusu Lissu, ndiyo ulaghai, uongo na utapeli wako unapojianika hadharani. Tazama matukio haya. Kwanza ulisimama Bungeni ukijitanabaisha kama Mfafanuzi wa idadi ya risasi aalizopigwa Lissu Septemba 7 mwaka 2017. Ukayasema uliyoyasema. Watu wakakutazama tu. Tena, ukasimama Bungeni na kusema kuwa Bunge limelipia matibabu ya Lissu. Ukawa ni uongo, ulaghai na utapeli wa mchana kweupe.

Halafu, ukasimama juzi hapa kusema kuwa Bunge halijui alipo Lissu na anachokifanya. Wewe huyohuyo ukasema Lissu anaonekana akizurura Ulaya na Marekani. Ukasema kuwa umeandika barua kwa Mwenyekiti wa NEC ukimfahamisha kuwa jimbo la Lissu liko wazi kwa sababu mbili. Moja ni kuwa hajulikani alipo na anachokifanya. Pili ni kuwa hakujaza fomu za maadili ya viongozi wa umma.

Tazama hapa: fomu za maadili ya viongozi hupaswa kuwasilishwa kila ifikapo tarehe 31 Disemba ya kila mwaka. Lissu, kutokana na shambulio lake, hakujaza fomu za mwaka 2017 na 2018. Sababu inajulikana: alikuwa mgonjwa aliyekuwa amelazwa nje ya nchi. Kuhusu yuko wapi, barua zilizoandikwa na Bunge kwa familia ya Lissu zinakuanika waziwazi. Si jambo jema kuishi kwenye uongo, ulaghai, utapeli na kutumika.

Sekretarieti ya Maadili ina taratibu zake; ina mamlaka yake na mipaka yake. Sekretarieti huchunguza tu. Haimkuti yeyote na hatia ya kukiuka sheria ya maadili. Kuna Baraza la Maadili lenye mamlaka hayo. Sekretarieti hushtaki hapo baada ya kuchunguza. Kitendo cha Bunge kuandika barua kuulizia tu kama Lissu amejaza fomu au la na kuhitimishja kuwa amekiuka sharia ni utapeli, ulaghai na uongo. Ni kutumika.

Nina mengi ya kuyaandika hapa lakini naomba niishie hapa kwasasa. Ieleweke kuwa utapeli, ulaghai na kutumika kuna mwisho mbaya sana.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)
Njaa mbaya baba, ngoja tumsubiri 2020 kama hatatupwa na hao anaowatumikia. Mwisho wake utakuwa mbaya na alivyo na hasira ataishia Jela. Bado muda mfupi sana
 
Ni huzuni kwa bunge
 
Mzee Tupatupa wa Lumumba najua unajua mengi Sana ambayo Sisi wengine hatujui naomba unijulishe na utuletee sheria na taratibu za mtumishi wa Bunge na Mbunge akiwa mgonjwa zinasemaje
Ukisha tuletea hapa kama zilivyo hapo tunaweza sema kitu,maana sheria za watumishi wengine wa serikali na sekta binafsi tunazijua
 
Sometimes I wonder whether the world is being run by smart people who are putting us on or by imbeciles who really mean it!!! Shame be unto whoever feels he hold the keys to peoples lives!
 
Ndugai ni mfano mbaya sana kwa viongozi waganga njaa na wanaojipendekeza kuliko maelezo. Anafanya mambo huku roho yake inapinga Dr. Mzima sijui elimu yake inamsaidia nini
 
huyu jamaa wa kongwa kwa sasa anakula na kusaza

na kaajiri mtumishi wa kutupa makombo kila siku jalalani..

yupo juu kileleni,na Labda madhila ya familia ya Mbunge wake yanamwongezea mileage huko kileleni
 
Naomba uniambie kwa miaka mitatu Nimrodi Mkono amelazwa na yeye amejeza? Ndugu yangu jaribu kuweka hapa ubinadamu kidogo. Hivi Lissu amekataa kujaza hizo form kwa makusudi au umeamua tu na wewe uonekane umeweka neno.
Pili sheria inasema mtu asipohudhuria mikutano mitatu ya bunge afukuzwe. Je kama sheria inafuatwa na Ndugai hajui alipo Lissu alitakiwa tangu mwaka jana mwanzoni wawe wamemtimua ubunge. Sasa je hapo aliyeandika kitu cha hovyo ni wewe au vuta- nkuvute? Jibu tu kwa upole wala usiweke hasira.
Unapoteza muda kujibizana na mdaka makombo!
 
Kwa vinyongo na visasi hivi, Tanzania si salama tena. Siioni taasisi yoyote inayoweza pooza machungu ya Watanzania hivi sasa, wala kwa kipindi cha karibuni. Nchi iliyoishi vema hapo awali, ipo njiani kuja kuunda kamati ya maridhiano kama South Africa na Rwanda. What a shame!!

Ili taifa lipone kisasi ni haki kama njia ya kulipa wote waliyotufikisha hapa.Kisasi ulipwa Kwa kisasi ndipo uponyaji huja.
 
Hakika huyu "agwe" atashikilia historia ya kuwa ni Spika wa hovyo kabisa aliyewahi kutokea pale Bungeni, tokea nchi hii iwe na maspika wa Bunge letu, tokea tupate uhuru

Hakika anatekeleza "maagizo" aliyopewa na Jiwe, "unafanya kazi nzuri sana ya kuwatimua hao wabunge wa upinzani Bungeni, ukishawatimua huko nami nitadeal nao huku uraiani" mwisho wa kunukuu

Hivi Jiwe anavyofikiri kwa kuwatumia hao Policcm, huku uraiani, kuwanyanyasa wapinzani ndiyo ujanja kweli??
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom