Spika Ndugai, hadi lini unajibanza kwenye uongo, ulaghai, utapeli na kutumika? Hufanani na uyafanyayo. Umepatwa na nini?

Kuongoza ni kuweka ukweli mbele. Ni kukumbatia na 'kushare' haki kwa unaowaongoza. Ni kufuata taratibu zilizopo huku ukitanguliza maslahi ya unaowaongoza, haki zao na wajibu wao. Kuongoza si kujitutumua, kujianika na kujichora kuwa una nguvu au una uwezo wa kuamua utakavyo. Uongozi si rafiki wa uongo, ulaghai na utapeli.

Spika Job Yustino Ndugai, umepotoka. Umejibanza kwenye uongo, utapeli, ulaghai na ni Dhahiri kuwa unatumika. Ninalazimika kuongea kwa uchungu na ukali kwako kada mwenzangu na kiongozi wangu wa CCM (najua unaingia Kamati Kuu ya CCM na mikutano mingineyo kwa nafasi yako). Amini nakwambia, ulikojibanza si sehemu salama wala hakutakusaidia.

Umekuwa ukiwatimua Bungeni Wabunge mbalimbali wa Upinzani ukisukumwa na hisia na kutaka kwako kuonekana kuwa wewe ni mtumishi muaminifu wa CCM na unayafanya yenye baraka za CCM. Katika hilo, umekuwa kila mtanzania ajue kuwa unawashughulikia wapinzani ndani ya Bunge(inadaiwa unatekeleza agizo la Mwenyekiti wetu alilolitoa Ikulu). Wapinzani wamekuwa wakikosa fursa ya kujitetea, kupata nafasi ya kufurukuta na kadhalika.

Kuhusu Lissu, ndiyo ulaghai, uongo na utapeli wako unapojianika hadharani. Tazama matukio haya. Kwanza ulisimama Bungeni ukijitanabaisha kama Mfafanuzi wa idadi ya risasi aalizopigwa Lissu Septemba 7 mwaka 2017. Ukayasema uliyoyasema. Watu wakakutazama tu. Tena, ukasimama Bungeni na kusema kuwa Bunge limelipia matibabu ya Lissu. Ukawa ni uongo, ulaghai na utapeli wa mchana kweupe.

Halafu, ukasimama juzi hapa kusema kuwa Bunge halijui alipo Lissu na anachokifanya. Wewe huyohuyo ukasema Lissu anaonekana akizurura Ulaya na Marekani. Ukasema kuwa umeandika barua kwa Mwenyekiti wa NEC ukimfahamisha kuwa jimbo la Lissu liko wazi kwa sababu mbili. Moja ni kuwa hajulikani alipo na anachokifanya. Pili ni kuwa hakujaza fomu za maadili ya viongozi wa umma.

Tazama hapa: fomu za maadili ya viongozi hupaswa kuwasilishwa kila ifikapo tarehe 31 Disemba ya kila mwaka. Lissu, kutokana na shambulio lake, hakujaza fomu za mwaka 2017 na 2018. Sababu inajulikana: alikuwa mgonjwa aliyekuwa amelazwa nje ya nchi. Kuhusu yuko wapi, barua zilizoandikwa na Bunge kwa familia ya Lissu zinakuanika waziwazi. Si jambo jema kuishi kwenye uongo, ulaghai, utapeli na kutumika.

Sekretarieti ya Maadili ina taratibu zake; ina mamlaka yake na mipaka yake. Sekretarieti huchunguza tu. Haimkuti yeyote na hatia ya kukiuka sheria ya maadili. Kuna Baraza la Maadili lenye mamlaka hayo. Sekretarieti hushtaki hapo baada ya kuchunguza. Kitendo cha Bunge kuandika barua kuulizia tu kama Lissu amejaza fomu au la na kuhitimishja kuwa amekiuka sharia ni utapeli, ulaghai na uongo. Ni kutumika.

Nina mengi ya kuyaandika hapa lakini naomba niishie hapa kwasasa. Ieleweke kuwa utapeli, ulaghai na kutumika kuna mwisho mbaya sana.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)
Ndugai ni shetani ambaye hata shetani mkuu anamshangaa. Leo anawezaje kusimama hadharani na kuomba huruma ya watanzania kana kwamba aliyoyatenda kwa Lissu hadharani ni sahihi?
Kama aliutendea vile mti mbichi tena ukiwa kwenye hali ile anao utu gani wa kutetewa. Hata Mungu atanishangaa. Avune alichopanda, kupalilia na kuwekea mbolea.
 
Back
Top Bottom