Spika Ndugai: Bunge limeazimia kutofanya kazi na Profesa Mussa Assad si ofisi ya CAG. Ripoti itasomwa endapo haijasainiwa na Prof. Assad

Spika wa Bunge, Job Ndugai ametoa ufafanuzi juu ya azimio la Bunge la kutokufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa Bunge limeazimia kutofanya kazi na kutoshirikiana na CAG na sio ofisi ya CAG. Kwa mantiki hiyo, ripoti itasomwa endapo haijasainiwa na ASSAD. View attachment 1062521

========

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema Bunge lilitangaza kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na si ofisi yake.
Ndugai ametoa kauli hiyo leo mchana Alhamisi Aprili 4, 2019 baada ya kuwatambulisha wageni walioalikwa bungeni, akiweka sawa hali ya sintofahamu iliyoibuka baada ya Bunge kutangaza kutofanya kazi na Profesa Assad.

“Hakuna wakati wowote ambao Bunge limekataa kufanya kazi na taasisi ambayo ni ofisi ya CAG. Bunge hili limekataa kufanya kazi na mtu anayeitwa Profesa Assad basi. Tusiripoti tofauti tukauchonganisha umma na kuuchanganya,” amesema Ndugai.

Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa Bunge ni dhaifu.

Chanzo: Mwananchi
Okay
 
Ndugai SUKUMA GANG enzi za unyapara wake.
 
Back
Top Bottom