Spika Ndugai: Bunge limeazimia kutofanya kazi na Profesa Mussa Assad si ofisi ya CAG. Ripoti itasomwa endapo haijasainiwa na Prof. Assad

Nelson Masaduki

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
346
380
Spika wa Bunge, Job Ndugai ametoa ufafanuzi juu ya azimio la Bunge la kutokufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa Bunge limeazimia kutofanya kazi na kutoshirikiana na CAG na sio ofisi ya CAG. Kwa mantiki hiyo, ripoti itasomwa endapo haijasainiwa na ASSAD.
spika.jpg


========

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema Bunge lilitangaza kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na si ofisi yake.
Ndugai ametoa kauli hiyo leo mchana Alhamisi Aprili 4, 2019 baada ya kuwatambulisha wageni walioalikwa bungeni, akiweka sawa hali ya sintofahamu iliyoibuka baada ya Bunge kutangaza kutofanya kazi na Profesa Assad.

“Hakuna wakati wowote ambao Bunge limekataa kufanya kazi na taasisi ambayo ni ofisi ya CAG. Bunge hili limekataa kufanya kazi na mtu anayeitwa Profesa Assad basi. Tusiripoti tofauti tukauchonganisha umma na kuuchanganya,” amesema Ndugai.

Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa Bunge ni dhaifu.

Chanzo: Mwananchi
 
Huko ni kuchanganya, wangesema hawataki kufanya kaz na Assad na siyo CAG.

Wakisema hawataki kufanya kaz na CAG ina maana hata akiteuliwa mwingine bado ni CAG hawatafanya kazi naye pia?

Duuh, hizi akili zangu hizi sijui zimenizidi au ndo nakaribia kutokomezwa ziro😎😎
 
Sijui mi ndo sielewi Kiswahili!!
  1. Kwani huyo CAG si anafanya kazi ndani ya ofisi ya CAG?
  2. Hivi ofisi ya CAG inaweza kufanya kazi bila kuwa na CAG?
  3. Hiyo ripoti imetolewa na CAG au na ofisi ya CAG? Najiuliza maswali mengi lakini huenda ni ujinga wangu tu.
 
So hiyo report itakuwa invalid kama tu imesainiwa na Prof Assad? The very report ambayo obviously yeye ndiye ataisimamia itakuwa valid kama itasainiwa na mtu mwingine. Some rubbish thinking of the lowest level, is speaker Ndungai really sane?

Who is behind this stupidity? I mean who is behind this whole ordeal?
Wawakilishi wa wananchi mpaka kufika kiwango cha kujitoa ufahamu kiasi hiki ni aibu na fedhea kwao na inadhihirisha jinsi viongozi wanavyoamini kuwa wananchi wanaowatawala ni mazoba kiasi kwamba they dance any tune from them.
 
Back
Top Bottom