Spika Ndugai: Bunge liangalie Sheria za Adhabu mambo ya kuwafunga watu miaka 10, 20 yamepitwa na wakati mwaka 1 unatosha kujirekebisha

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,834
141,755
Spika Ndugai ameshauri kamati ya bunge ya sheria kuangalia upya sheria za adhabu kwa sababu huko duniani vifungo vya miaka 10, 15 20 wameshaachana nazo kwa sababu dunia inakwenda kasi sana.

Ndugai amesema kwa kasi ya sasa ya dunia kifungo cha mwaka mmoja kinatosha kabisa kumrekebisha mtu.

Chanzo: ITV habari
 
Kifungo kirefu kiwe mwisho 25 years, hapo tutakuwa binadamu haswa. Mambo ya life and death sentence ni ushamba.
 
Ukiona hivyo hapo kuna mtu wake wa karibu kanyeshewa mvua na hana cha kuepusha kama yeye atakavyoshitakiwa hapo baadae
 
Spika huyu hana akili.

Huko kwa wenzetu ndio mtu anafungwa miaka 200, miaka 300, 4 or 5 life sentences yeye anasema miaka 10 imepitwa na wakati? Hivi huyu ana akili kweli?

Lock them criminals for life or execute them.

Mtu anabaka mtoto wa miaka 3 afungwe mwaka mmoja? Mtu anaua albino afungwe mwaka atoke aendelee kuua albino? Mtu aue wazee na vikkngwe kwa sababu zake afungwe mwaka mmoja aachiwe aje kumaliza wazee?

Mtu anaua watu 5 ama zaidi, afungwe mwaka mmoja aachiwe kuja kuua tena?

Yeye pale spika mtu akimvamia kwake akamlawiti na kuwanajisi watoto wake mbele yake atafurahi huyo jamaa kufungwa mwaka mmoja na akaachiwa ama atamuombea kabisa asifungwe?
 
Ushindi mtupu, amekiri kuwa all are defective charges and ought to be dismissed, lkn kwa vile ana maagizo afanyeje ndiyo maana ame concede resignation in the midst of the court session
Hahahaaaa!! Mungu awape wepesi mtani!
 
Naungana na Ndugai kwa nini mtu afungwe miaka mingi kwa makosa ya kawaida kabisa..mbaya zaidi wanaofungwa ni wale wasio na uwezo wa kuhonga.
 
Mkuu yule dhalimu mwendazake angekuwa hai huyo MNAFIKI asingeongea haya. Yule dhalimu alitaka wafungwa wasilale lupango wafanyishwe kazi kwa masaa mengi na pia wawe wanapigwa na huyo mnafiki hakutia neno?
Inawezekana shetani akizeeka akawa malaika?
 
Back
Top Bottom