Spika Ndugai azitega Kamati za Bunge, azitaka ziache kufanya kazi kwa mazoea

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,776
2,000
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameziagiza kamati za kudumu za Bunge, ziache kufanya kazi kwa mazoea na kubweteka, zikiamini muda bado upo, hali inayoweza kusababisha zimalize miaka mitano bila kufanya lolote kusaidia na kuishari serikali kwa manufaa ya taifa.

Ndugai alitoa agizo hilo bungeni jana jijini Dodoma wakati akisitisha shughuli za Bunge. Alizitaka kamati hizo kwenda na kasi katika utendaji wake na kuwatumia vyema mawaziri waliopo na kuhakikisha wanaanza na mambo ya msingi, ambayo wajumbe wa kamati hizo ambao pia ni wawakilishi wa wananchi wanayataka yatekelezwe.

Alitoa mfano wa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii na kuitaka kwenda kasi hususani katika eneo la bima ya afya kwa wote, jambo ambalo lina manufaa kwa Watanzania ambao ni wapiga kura na lenye maslahi kwa taifa.

Alisema kuna majukumu yanayopangwa na Spika kwa kamati na yapo pia majukumu ambayo kamati hizo, zinapaswa kujipangia na kuyatekeleza wenyewe kikamilifu, kwani jukumu lao ni kulishauri Bunge na serikali kwa ujumla.

Alisema Ofisi ya Bunge iko tayari kutoa ushirikiano na msaada wowote, ambao kamati hizo zitahitaji katika kutimiza majukumu yao kikamilifu.

“Nawaambia yapo baadhi ya malengo ambayo msipojipanga vizuri ndani ya miaka mitano yanaweza yasifikiwe. Bima ya afya kwa wote, kamati ya huduma ya jamii, mkichekacheka miaka mitano itakwisha hiyo Sheria haijafika hapa bungeni, lazima muanze ufuatiliaji wa kutosha katika kila hatua, toeni ushauri wa namna gani jambo hilo litafanikiwa,” alisema Ndugai.

Aidha, aliitaka kamati hiyo pia kusaidia katika suala la mabadiliko ya mtazamo katika elimu, ambapo kuna haja kubwa ya kamati kuonyesha muono wao na kushauri serikali katika eneo hilo na si lazima wasubiri mijadala ya kitaifa.

“Kiukweli watoto wetu wanasoma masomo akirudi huna pa kumpeleka naye hana cha kufanya, kwanini tusielekeze nguvu zetu nyingi katika maeneo ambayo mtoto anaweza kujiajiri na kuisaidia nchi katika uchumi wa kati, kuweza kwenda mbele na hawezi kulala njaa kwa kukosa kazi au ajira hata siku moja,”alisema.

Alisema kuwa badala ya kuwa na shahada ambazo hazina tija, ni heri watoto wakapata fani mbalimbali ambapo mtu mmoja anaweza kuwa na fani zaidi ya moja, tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi wanamaliza vyuo wanasubiri tu kuajiri.
 
  • Wow
Reactions: Lob

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
9,501
2,000
Hata spika pia ubadilike sasa ni wakati wa bunge live wale wahuni wa kutafsiri vifungu vya biblia hawapo tena!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom