Spika Ndugai adai tena kuwa Lissu alishalipwa pesa zake zote

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,897
SPIKA NDUGAI: HAKUNA ANAYELIDAI BUNGE, "KAMA MTU AMEISHIWA HUKO ULAYA SI ASEME"

Spika wa bunge Job Ndugai amewaonya wanaotoa taarifa za upotoshaji zenye lengo la kulichafua bunge kuacha kufanya hivyo kwa kuwa sasa hatua zitaanza kuchukuliwa ikiwemo kuitwa kwenye kamati ya maadili ya bunge

Spika Ndugai ameyasema hayo bungeni Dodoma leo Juni 25,2021 wakati akitolea ufafanuzi wa orodha inayozagaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha majina ya waliokuwa wabunge wa bunge la 11 likiwemo la Tundu Lissu kuwa wanalidai bunge hivyo walipwe

Spika amesema taarifa hiyo ni ya uongo kwa kuwa ilikuwa ya mwaka 2018 na kwamba hakuna mbunge wala aliyekuwa mbunge hata mmoja anayelidai bunge

"Na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu, ila zilipoingia benki walizichukua zote, na kama mtu kaishiwa huko ulaya alipo si aseme tu, bunge ni taasisi iliyopo makini na haimuonei mtu, hakuna hata mmoja anayeidai" amesema Spika Ndugai

==========

"Na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu, ila zilipoingia benki walizichukua zote, na kama mtu kaishiwa huko Ulaya alipo si aseme tu, Bunge ni taasisi iliyopo makini na haimuonei mtu, hakuna hata mmoja anayeidai"

Amesema Spika Ndugai

===========

Spika Ndugai akiwa Bungeni leo Ijumaa Juni 25, 2021 amekanusha Tangazo lilitoka na kuelezea madai ya wabunge wanaolidai Bunge.

Spika Ndugai: Jana kuna tangazo fulani lilitoka la majina mengi kwamba limetolewa na TRA, katika majina yale mengi ya wizara mbalimbali yapo na majina ya wabunge wa Bunge la 11 lililomaliza muda wake.

Kumbe lengo lao ni kumfatilia mtu mmoja tu wanayemtaka wao kuonyesha ana madai fulani bungeni lakini Orodha imetolewa ndefu na wakaanza kumshambulia Spika na kuchonganisha na kadhalika.

Tangazo hilo ni la uongo, ni tangazo lilikuwa la mwaka 2018 huko nyuma na malipo hayo yalisharekebishwa na niwaambie wabunge wa Bunge ambalo limemaliza muda wake maana wengine hali ni mbaya huko, sasa walipoona lile tangazo, simu ya spika imejaa bwana tuna madeni tunadai kwako.

Hakuna anaedai Bunge, hakuna. Katika chombo ambacho kinafanya kazi vizuri, kimojawapo ni bunge. Hakuna anaedai na kama mtu ameishiwa huko Ulaya au wapi si aseme tu kuliko kusingizia Bunge kila wakati kwamba kuna madai, hakuna anaedai, hayupo na hata huyo mtu wao alilipwa kila kitu.
 
Bunge linalojadili kujiongezea posho ni bunge takataka kabisa.

Kila taasisi wakianza kujadili kuongezewa mishahara wakati wa kazi.

Kazi zitafanyika?

Yule mbunge alishindwa nini kupeleka mapendekezo yake kwenye mamlaka zinazohusika na mishahara.

Ndungai ni takataka na Bunge ni takataka kabisa
 
FB_IMG_16182418594249922.jpg
 
Maneno ya mkosaji
Kama la akina Mbowe limetenguliwa basi aamini hata yaliyopo bungeni yatatenguliwa
Asijitutumue kuona ni mungu mtu
Wakati wa majigambo dharau kebehi unayoyoma
Katiba Mpya itakuchakaza mpaka utoke kinaniii
Kuwa mpole utajiepusha na mengi ndunga yai
 
Naunga mkono hoja ikiwezekana waitwe na wapewe adhabu ya kuchapwa viboko hao wazusha ikiwemo mmachame Mallisa
 
Ungenyamaza tu,Hekima si kila kitu uongee.Uwe unatoka nje ya hicho kiti unapotaka kuongelea jambo ambalo chanzo ni matandao ili waandishi wa habari wapate kukuuliza maswali kubalance story.
MAMA HAPENDI SHOBOSHOBO
 
Back
Top Bottom