Spika Ndugai awapongeza Wakenya kwa kuonesha mubashara Vikao vya Kamati vya Bunge

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,454
3,418
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewapongeza Wakenya kwa Kuonesha Mubashara Vikao vya Kamati vya Bunge

Amesema “Nawapongeza kwa uzinduzi, kwamba sasa vikao vya kamati mbalimbali vitapeperushwa mubashara (Live)”

Aidha, amewasihi kutumia Kiswahili kwani inawezekana kama kinavyotumika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Ndugai yupo Jijini Nairobi, katika Uzinduzi wa Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya (Standing Orders) kwa lugha ya Kiswahili
 
Muache awapongeze wakenya hajui tembo wamejaa sumu wako dodoma wanaenda kubomoa bunge!
 
Kama kweli kuna hukumu ya mwisho baada ya maisha ya duniani basi wanasiasa watakaochomoka ni wachache mno.
 
Mimi nampongeza Ndugai kwa kupongeza Bunge la Kenya live wakati la kwake hataki hata kusikiia neno LIVE
Heko speaker wetu kwa busara zako zilizotukuka. Big up sana.
Jamani, tusibadirishe historia; hivi ni yeye (spika ) ndiye aliyetaka bunge lisiwe live? Tusije kumuonea mgogo wa watu
 
Back
Top Bottom