Spika Ndugai awaonya upinzani wasifukuze wabunge, awataka wajifunze kutoka CCM!

Acha wafukuzane! Mgogoro wa Ccm 2007-2015 kama wangefukuzana basi leo hii ingebaki historia
 
Kama hujui, ccm ndio mabingwa wa kuingiza mamluki kwenye vyama vya upinzani ili kuleta migogoro na kuvisambaratisha. Sasa kusipokuwa na nguvu ya uongozi kuwaondoa ujue ndio mwisho wa vyama pinzani Tanzania.
Wabunge wanaofukuzwa upinzani ni mapandikizi ya CCM spika lazima alalame kupoteza watu wao.
 
Matatizo ya CCM sio sawa na ya vyama pinzani..... sioni ccm kiongozi/mwenyekiti anajiuzulu harafu analazimisha kurudi wakati aliye mkimbia akiwa bado yupo na anapata support ya baadhi ya wabunge.... kulinganisha ccm na upinzani upande wa matatizo yao ni makosa makubwa. .. mbingu na dunia..
 
Ficha ukilaza wako, Mansoor hajawahi kuwa mbunge, alishawahi kuwa mwakilishi tu wa baraza la wawakilishi Zenji.
kwani alikuwa anatoka chama gani? halafu kumbe mwakilishi wa baraza la wawakilishi sio sawa na mbunge?
ELIMU,ELIMU,ELIMU.
 
Kuna udikteta mkubwa sana kwenye vyama vya upinzani kuliko hata huo wanaouita udikteta uchwara.

Vyama vya upinzani vina wenyeviti na makatibu wakuu wa kudumu kama Mbowe. Mrema,Cheyo,maalim Seif, Mbatia nk.
Ukikosana na mwenye chama lazima ufukuzwe hakuna Uhuru wa maoni wala demokrasia.
Hao ni wafalme, sio wenyeviti wa vyama. Haiwezekani mtu huyo zaidi ya miaka ishirini ni katibu wa chama, zaidi ya miaka kumi ni mwenyekiti wa chama...then wanajiita "demokrasia na maendeleo"...
 
Mansoor Himid Yusuf
Mwakilishi wa Kiembe SamakiCCM- ZNZ mbona alifukuzwa?
Ndugai bana au bado hajapona?
 
Wewe Baraza la Wawakilishi ZNZ ndiyo Bunge la ZNZ
Kama muungano utavunjika hawa wawakilishi wa majimbo watabaki lkn wabunge toka ZNZ watafutwa
 
Kuna udikteta mkubwa sana kwenye vyama vya upinzani kuliko hata huo wanaouita udikteta uchwara.

Vyama vya upinzani vina wenyeviti na makatibu wakuu wa kudumu kama Mbowe. Mrema,Cheyo,maalim Seif, Mbatia nk.
Ukikosana na mwenye chama lazima ufukuzwe hakuna Uhuru wa maoni wala demokrasia.
Lipumba alikosana na nani wakati yeye ndio aliekuwa mwenyekiti? Kwanini asimfukuze huyo aliekosana nae na badala yake akakimbilia kujiuzulu? Sasa leo hii analeta vurugu eti anataka arudishiwe uenyekiti bila uchaguzi bila utaratibu wowote halafu nyie maluki mnamtetea. Tuachane na siasa, Hivi hata mke wako akikuacha na akaondoka kwako kwa sababu zake binafsi then baada ya mwaka anarudi anakwambia mimi ndio mke wako nimerudi nyumbani kwangu na naitaka nafasi yangu bila masharti wala kujadiliwa, utampokea na kuendelea na maisha?
HATA UKIMWI HATAKI MKAPIME.
Acheni kujitoa ufahamu bhana mnajishushia hadhi kusimamia uovu.
 
Vipi kuhusu Mansoor aliyefukuzwa ccm na kuvuliwa ubunge??
Either Kuna baadhi ya kumbukumbu zimebaki India kama bond ili akimaliza kuliipa deni la matibabu watamrudishia au, ramani yake kichwani kuhusiana na Tanzania huwa haifiki Zanzibar.
 
Kwa hiyo Lowassa,Sumaye,Kingunge ni mamluki?
Uwe na uelewa hata kidogo basi, aliesema hao ni mamluki ni nani? Wangekuwa mamluki wangeshatimuliwa. Yeyote unaeona katimuliwa kwa misingi ya kukisaliti chama ujue ni mamluki.
Na mamluki sio lazima atoke chama kingine kuingia kingine, bali hata walioanza na chama hichohicho wanaweza kununuliwa na kupandikizwa kama mamluki na wakaanza kukihujumu chama. Taja Slaa, Taja Lipumba, Taja Zitto ongeza na wengine alafu uliza.
 
Kwa michango ya humu, na kama haya ndio mawazo yaliyomo vichwani mwa Waheshimiwa Wabunge, basi sitashangaa nikisikia kwamba kuna Kundi la Wabunge wametoka Bungeni wakimpinga Spika Job Ndugai kwa kuingilia maamuzi ya vyama vyao, na wakishinikiza aje Naibu Spika ili awaongozee baraza. Ndivyo tulivyo.
 
Uwe na uelewa hata kidogo basi, aliesema hao ni mamluki ni nani? Wangekuwa mamluki wangeshatimuliwa. Yeyote unaeona katimuliwa kwa misingi ya kukisaliti chama ujue ni mamluki.
Na mamluki sio lazima atoke chama kingine kuingia kingine, bali hata walioanza na chama hichohicho wanaweza kununuliwa na kupandikizwa kama mamluki na wakaanza kukihujumu chama. Taja Slaa, Taja Lipumba, Taja Zitto ongeza na wengine alafu uliza.
Ungemsoma kwanza aliyem-quote nadhani ungeipata point yake
 
Zito alikuwa msaliti! Hilo ni kosa kubwa! Ni kama kupindia nchi! Alitaka kumpindua Mbowe. Ya sakaya yanasameheka maana yeye anampenda lipumba, siyo kosa!
Kwani mbowe yeye hatakiwi kupingwa? Yeye ni mfalme wa chadema hivi vyama vya upinzani ni tatizo kubwa sana,

Naamini demokrasia ya kweli itashamiri nchini pale.tu hata vyama vya siasa vitakapokubali kuongozwa kidemkrasia.

Vinginevyo ni kuwahadaa wananchi.
 
Mbowe lazima apingwe, lakini siyo kwa kufanya mipango ya chini chini kumpindua. Kama Mbowe alikataa wengine wasigombee uenyekiti, then, hilo nalo ni kosa.
Upande mwingine, vyama hivi vinajijenga , vinapigwa vita sana na serikali, visipopata mtu wa kujitoa mhanga/kuvitetea bila woga as long as huvunji sheria, CCM itavifuta. Mtu mwoga kama Zito angelihimili mikikimikiki ya sasa wanayopitia CDM. Walimtishia tu, akanyamaza na sasa anaomba fadhila za bwana Mkubwa badala ya kudai haki yake!
 
Back
Top Bottom