Spika Ndugai awaapisha Humphrey Polepole na Riziki Lulida. Asema Bunge linawatambua Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofutiwa uanachama CHADEMA

Nafasi kumi alizopewa Rais na Katiba ya JMT ni kama katika wabunge waliopo hakuna mtu ana sifa anazotaka lakini sio mBunge ndio anateua sasa huyu wetu anateua watu wa ovyoovyo ili kujaza makasuku kule mjengoni shida
Acha wivu, tumia watu walitumikie taifa, hata wewe ni wa ovyo ovyo lakini ukiteuliwa huwezi kataa, so wivu unakusumbua tu
 
Spika wa Bunge Job Ndugai leo November 30,2020 atawaapisha Wabunge wawili walioteuliwa na Rais Magufuli, Wabunge hao ni Humphrey Polepole ambaye ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Riziki Said aliyekuwa Mbunge Viti Maalum katika Bunge la 11 kupitia CUF.

Shughuli za uapisho zitafanyika katika Viwanja vya Bunge Jiji Dodoma saa 10:00 Jioni.


 
Huyu mama aliekuwa m'bunge wa KAFU ameunga mkono juhudi za meko au ni meko kujipendekeza.
 
Huku ni kuongeza gharama za bure, si wangeapishwa pamoja na wale COVID- 19 leo.
 
Kuna jambo kweli halipo sawa katika Nchi yetu, hivi kweli uvunjifu mkubwa wa katiba uliofanyika Spika wa Bunge anakuja na utetezi mwepesi kiasi hichi.

Kuna haja ya kujitafakari kama nchi kujua tulipojikwaa ili tuanze upya la sivyo Kuna hatari kubwa sana mbele yetu.

Mungu ibariki Tanzania
 
Yani ni juzi tu Polepole kateuliwa usiku wa manane kuamkia jumapili. Halafu leo anaapishwa. Haraka haraka ya nini wanakimbia wapi?

Wakati vifungu vya Katiba vimeweka wazi mtu akiteuliwa na rais lazuma wiki ipite kwanza ili aapishwe Wananch wajiridhishe kusikuwe na sintofaham. Vifungu vya katiba viko wazi kabisa kuhusu swala hili.

Kwanini wabake katiba yetu?
 
Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Bi Magreth Thacher alupofariki kuna kundi la watu walipita barabarani kusheherekea kifo chake, nilikuwa sijawaelewa lakini sasa nimewaelewa.

Hata Tanzania kuna watu siku ya kifo chao Taifa litakuwa kwenye furaha na kuchoma nyama na kunywa pimbe kusheherea vifo vyao.

Wekeni hii comment kwenye kumbukumbu zenu, tena mmoja kiafya wala hana maisha marefu.
 
Wabunge wote wa Bunge la 12 tulioowaapisha tunaendelea kuwatambua kwamba ni wabunge kamili ikiwa ni pamoja na wale 20 wa chama cha CHADEMA”Spika Ndugai
 
Nafasi kumi alizopewa Rais na Katiba ya JMT ni kama katika wabunge waliopo hakuna mtu ana sifa anazotaka lakini sio mBunge ndio anateua sasa huyu wetu anateua watu wa ovyoovyo ili kujaza makasuku kule mjengoni shida
Katiba haielekezi unavyotaka wewe.

Rais amepewa uhuru kuchagua mtu yoyote mwenye sifa za kuwa mbunge, hata akichagua mjomba wako Mbowe hakuna anaeweza kumuhoji kwa sababu habanwi na katiba.
 
Yani ni juzi tu Polepole kateuliwa usiku wa manane kuamkia jumapili. Halaf leo anaapishwa. Haraka haraka ya nini wanakimbia wapi? Wakati vifungu vya Katiba vimeweka wazi mtu akiteuliwa na rais lazuma wiki ipite kwanza ili aapishwe Wananch wajiridhishe kusikuwe na sintofaham. Vifungu vya katiba viko wazi kabisa kuhusu swala hili.

Kwanini wabake katiba yetu?
Mungu usikia kilio cha wenye haki, kuna watu wanasumbuliwa na kiburi cha uzima.
 
Waliosusia matokeo ndio wamekuwa wafuatiliaji wakubwa wa shughuli za Bunge, mpaka ikifika february 2021, mtakua na alcers.
 
Ukuwa makini sana kwa siasa za Tz unaweza ukachizi bure. Lini speaker wa CCM amuonee huruma Halima mdee eti alivujika mkono kwajili ya Mbowe, wakati nyie CCM ndo mliwavunja duh
Kumvunja wamvunje wao leo wamuonee huruma, kwa kweli tuliambiwa kua uyaone ndiyo haya.
 
Back
Top Bottom