Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
MADINI YA TANZANITE: Spika wa Bunge, Job Ndugai leo ameunda kamati ya watu tisa itakayofanya uchunguzi katika uchimbaji na biashara ya madini ya Tanzanite.[HASHTAG]#MwananchiLeo[/HASHTAG]
======
======
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai jana tarehe 02/06/2017,ameteua kamati maalumu ya Bunge ya Wabunge 9 itakayochunguza Sekta nzima ya Madini ya Tanzanite.Spika ameiteua kamati hiyo leo Mjini Dodoma akiwa mwishoni kuahirisha kikao cha leo cha jioni cha Bunge mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Akitoa maelezo mbele ya wabunge Spika alisema kuwa ametumia kanuni ya 5 ,kanuni ndogo ya kwanza ya kanuni za kudumu za Bunge toleo la January 2016 inayompa uwezo wa kuunda kamati yoyote ili kuleta ufumbuzi wa jambo fulani ambalo ataikabidhi serikali kwa hatua zaidi za utekeleza spika ameipa siku 30 kamati hiyo ambayo imesheheni wataalamu mbali mbali wa kada zinazoendana na zoezi lililombele yao wa vyama pinzani na Chama Tawala ambao wataanza kazi rasmi mapema mwezi ujao wa saba mara baada ya vikao vya Bunge la bajeti kuahirishwa .
Kazi za kamati hiyo ni nyingi pamoja na hizi zifuatazo ambazo alizitaja Mhe Spika kwenye taarira yake ya Uteuzi.
1.Kuchambua mkataba kati ya shirika la Madini la Taifa maarufu kwa jina la State Mining Cooperation (STAMICO) na Kampuni ya Madini inayojulikana kama Tanzania One Mining Limited (TML) kwa lengo la kubainisha manufaa na hasara ambazo Nchi inapata kutokana na Mkataba huo.
2.Watathmini mfumo wa Uchimbaji, usimamizi na udhibiti wa biashara ya Madini ya Tanzanite ili yaweze kuchangia ipasavyo kwenye uchumi wa Taifa.
3.Kuchambua taarifa za tume mbali mbali na kamati mbali mbali ambazo zimewahi kuundwa na serikali huko nyuma kwaajili ya kushughulikia maboresho ya Madini ya Tanzanite na Mapendekezo yake kuona namna ambavyo utekelezaji wake umekuwa.
Majukumu hayo matatu ni majukumu Mazito na ya kizalendo ambayo tunaamini kamati itayatendea haki majukumu hayo.Tukumbuke tu Tanzanite inathamani zaidi ya Dhahabu.
Mara baada ya kukabidhiwa ripoti Mhe Spika ataikabidhi kwa Waziri Mkuu tayari kwa hatua stahiki kuchukuliwa.
Kamati ya Mhe Spika ni Mwendelezo wa Kamati ya kizalendo kama ile ya Prof Mruma iliyoteuliwa na Rais Magufuli.Ama kwa hakika viongozi wetu wameamua kusimama kidete kuyasimamia maslahi ya Nchi kwanza kuliko wao wenyewe.
Muda si mrefu naona wale wauzaji wakuu Duniani wa Tanzanite ya Tanzania South Africa na Kenya wakiingia kwenye wakati mgumu kwani wazalendo watachunguza kizalendo na kuamua kizalendo juu ya hatma na mwenendo wa uchimbaji wa Madini yao.
WAJUMBE WA KAMATI TEULE NI
1.Mh Doto Biteko Mwenyekiti wa Kamati hii teule na ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
2.Mh Mohammed Mchengerwa
3.Mh Ezekiel Maige
4.Mh Balozi Adadi Rajabu.
5.Mh Dkt Merry Mwanjelwa
6.Mh Subira Mgalu
7.Mh Juma hamad Omari
8.Mh Abdalla Mtolea
.9.Mh Joseph Ole millia