Spika Ndugai aumizwa na chama cha siasa kutoleta Wabunge wa Viti Maalum, adai zingekuwa nafasi za wanaume wangelishafika

Mapema leo spika Bunge, Job Ndugai alizielezea kamati za bunge na kusema wataziunda bunge lijalo kwa sababu serikali itakuwa imeshatengenezwa, pia akaongelea vyama ambavyo bado havijaleta wabunge japo wana fursa hizo hasa wabunge wa viti maalum ambapo makundi yaliyo bado ni matatu, mengine yakiwa wabunge watano kutoka baraza la wawakilishi Zanzibar na wabunge 10 wa kuteuliwa na Rais.

Ndugai: Viti Maalum kupitia vyama vya siasa, viko vyama bado havijatuletea wabunge wao, tunachoona kwenye mitandao na mahali pengine eti wanalumbana eti wasiwalete sijui wawalete, yaani ni ajabu, aibu kubwa sana kwa vya vya namna hii.

Ndio hawa tunaosema, kwa sababu ni fursa za kina mama wanalumbana wasije, zingekuwa hizo nafasi za wanaume wangeshafika siku nyingi, hao hao.

Sasa wapiga kura wakina mama nchi nzima ndio mzidi kuvielewa hivi vyama, ni shida. Wewe unawaziabiaje kina mama wasije kutetea watanzania humu ndani, ni jambo ambalo halikubaliki kabisa, kwanza haipaswi kuwa hata ni mjajadala lakini sasa ndio mzidi kuwaelewa, tunawaambia tu Februari hii ndio tunaanza, tukianza kwa utaratibu huo madongo yatakuwa mazito, wajitahidi mambo mengine wapunge punguze kidogo.

Vipo vitu sio vya kubishania kwa sababu ile ni fursa ambayo ni viruri kuitumia, ukiitupa vema wala hatuna shida kwa sababu hapa tunayo quorum, tuna kila kitu, tunaendelea.


Nafasi Nyengine awape lile Jeshi la kukodi kutoka Burundi
 
Bunge tunataka liwe la CCM tuwe na maendeleo kama Ulaya wapinzani wanatuchelewesha au Ndugai anapishana na bosi wake Rais Magufuli?

Huku Zanzibar CCM waliachiwa miaka mitano , hakuna chochote cha maana walichokifanya zaidi ya kuifisidi nchi na kuirudisha nchi miaka 200 nyuma
 
Hakuna hata wachawi wamloge huyu babu?
Ohoo, yeye mwenyewe ni mchawi wa kutupwa. Kilangila.
Nilichogundua kwa utafiti mdogo sana , watanzania hawana furaha baada ya matokeo na hata first lady nae vivyo hivyo. Ila chama dola hawaamini kilichotokea na nadhani hawakujipanga kujua kwamba chama pinzani wamejipanga haswaaa.
Ila chama pinzani strategy zao kubwa sana za kimataifa.
Kuchanya kutali. Kilangila.
 
Yeye alisema wapinzani hawatazidi wa tatu sasa anataka nini zaidi.​
 
Ndugai: Viti Maalum kupitia vyama vya siasa, viko vyama bado havijatuletea wabunge wao, tunachoona kwenye mitandao na mahali pengine eti wanalumbana eti wasiwalete sijui wawalete, yaani ni ajabu, aibu kubwa sana kwa vya vya namna hii.
Unapokuwa mtu mzima na umri kama wa ndugai unatakiwa uwe makini na unayoongea na kuacha unafiki na umuogope Mungu;
1. Wabunge 'waliodhulumiwa' haki zao ktk majimbo kwa 'kupokwa ushindi' wao mbona hao hasikitiki na kukemea?
2. wabunge wa viti maalamu mbona linamuuma?
*wenye akili eleweni namna wanasiasa wetu walivyo na tabia za ajabu!
 
Back
Top Bottom