Spika Ndugai aumizwa na chama cha siasa kutoleta Wabunge wa Viti Maalum, adai zingekuwa nafasi za wanaume wangelishafika

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,787
Mapema leo spika Bunge, Job Ndugai alizielezea kamati za bunge na kusema wataziunda bunge lijalo kwa sababu serikali itakuwa imeshatengenezwa, pia akaongelea vyama ambavyo bado havijaleta wabunge japo wana fursa hizo hasa wabunge wa viti maalum ambapo makundi yaliyo bado ni matatu, mengine yakiwa wabunge watano kutoka baraza la wawakilishi Zanzibar na wabunge 10 wa kuteuliwa na Rais.

Ndugai: Viti Maalum kupitia vyama vya siasa, viko vyama bado havijatuletea wabunge wao, tunachoona kwenye mitandao na mahali pengine eti wanalumbana eti wasiwalete sijui wawalete, yaani ni ajabu, aibu kubwa sana kwa vya vya namna hii.

Ndio hawa tunaosema, kwa sababu ni fursa za kina mama wanalumbana wasije, zingekuwa hizo nafasi za wanaume wangeshafika siku nyingi, hao hao.

Sasa wapiga kura wakina mama nchi nzima ndio mzidi kuvielewa hivi vyama, ni shida. Wewe unawaziabiaje kina mama wasije kutetea watanzania humu ndani, ni jambo ambalo halikubaliki kabisa, kwanza haipaswi kuwa hata ni mjajadala lakini sasa ndio mzidi kuwaelewa, tunawaambia tu Februari hii ndio tunaanza, tukianza kwa utaratibu huo madongo yatakuwa mazito, wajitahidi mambo mengine wapunge punguze kidogo.

Vipo vitu sio vya kubishania kwa sababu ile ni fursa ambayo ni viruri kuitumia, ukiitupa vema wala hatuna shida kwa sababu hapa tunayo quorum, tuna kila kitu, tunaendelea.
 
Spika kasema Kuna maneno uteuzi wa akina mama viti maalumu vyama vya upinzani kwa akina mama.

Spika kaonya wabunge viti maalum upinzani wajihadhari na rushwa isiyoeleweka kuwa wataeuliwa huko vyama vyao wakijirahisisha kirushwa wasije kwenda kumshtakia wakikosa kuwa ohh Mimi Kuna Rushwa isiyoeleweka mtu asiseme ooh nilitoa rushwa isiyoeleweka na chama hakikuniteua.

Kasema ndio maana Kuna ucheleweshaji Kuna maneno huko vyama vya upinzani.
 
Ndugai: Viti maalum kupitia vyama vya saisa, viko vyama bado havijatuletea wabunge wao, tunachoona kwenye mitandao na mahali pengine eti wanalumbana eti wasiwalete sijui wawalete, yaani ni ajabu, aibu kubwa sana kwa vya vya namna hii.
Kwani huwa anapita na kusoma JF?
 
Sasa anaumia nini huyu ndu.guy wakati hicho ndicho bosi wake (Jiwe) anachokitaka?! Kwamba wawepo CCM peke yao mjengoni kwa kuwa wapinzani wanazuia maendeleo!

Namshauri wabadili kanuni bungeni nafasi zote wajaze CCM kusudi nchi tupate maendeleo.
 
Spika kasema Kuna maneno uteuzi wa akina mama viti maalumu vyama vya upinzani kwa akina mama

Spika kaonya wabunge viti maalum upinzani wajihadhari na rushwa isiyoeleweka kuwa wataeuliwa huko vyama vyao wakijirahisisha kirushwa wasije kwenda kumshtakia wakikosa kuwa ohh Mimi Kuna Rushwa isiyoeleweka nilitoa na chama hakikuniteua

Kasema ndio maana Kuna ucheleweshaji Kuna maneno huko vyama vya upinzani
NDIYOOOOOOOOOOOO ya kwanza ndani ya bunge hili liliimbwa saa 6:59 (12:59pm).
 
Kasema ucheleweshaji kuwateua kwa visingizio vya kutunga Kuna lengo baya la rushwa isiyoeleweka
 
Back
Top Bottom