Spika Ndugai atangaza kutambua Ubunge wa Cecil Mwambe aliyejiuzulu Ubunge na uanachama CHADEMA

Hii nchi ina maajabu sana, pamoja na mbunge tajwa hapo juu aliekuwa akiwakilisha jimbo la Ndanda kupitia CHADEMA kutangaza kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM lakini bado anaendelea kupata stahiki zote kama mbunge na Ndugai bado anamtambua kuwa Cecil Mwambe ni mbunge wa Bunge la Jamhuri.

Kitendo cha Mwambe kuhamia CCM kilimpotezea sifa ya kuendelea kuwa mbunge, Hili la leo Spika wa Bunge amedhihirisha udhaifu alionao. Spika ni dhaifu na Bunge la 11 ni Bunge dhaifu mno katika historia ya Tanzania.

Nchi hii bunge lipo chini ya serikali, Mahakama inafuata maagizo ya serikali kufunga wasiowapenda. Huyu mbunge alishaacha ubunge na bunge likaridhia sasa baada ya watu kugundua kuwa bado analipwa mshahara, marupurupu na mkopo wake....Spika Ndugai akaona amefanya kitu ambacho sicho sahihi kwa hiyo njia yake rahisi ni kujifanya kutotambua barua yake ya kujiuzulu au ya katibu mkuu wa CHADEMA. Ndiyo hayo hayo ya Lipumba kujiuzulu halafu baada ya mwaka anatengua barua yake mwenyewe. NCHI HII NI YA AJABU.
 
Nyinyi wenye afya ya akili mbona mmefanya ya kijinga?
Suala dogo tu la kuambatanisha nakala za barua moja ya cecil mwambe kujitoa chadema na ya pili nakala ya barua rasmi ya kikao halali kilichomtoa au kumjadili na kuamua rasmi kutomtambua kama mwanachama wenu?

Mnarudia makosa yaleyale mliyoyafanya ya kutomtambua joseph selasini kama mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa maandishi.

Chadema mnakwama wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mtu amejivua mwenyewe uanachama. Ulitaka kikao kikao kikae kujadili nini? Kumuomba arudi au? Yaani hata kutofautisha mtu kujivua uanachama na kufukuzwa uanachama hamuwezi.

Hivi hizi ndio akili za ccm? So sad.
 
Hii nchi ina maajabu sana, pamoja na mbunge tajwa hapo juu aliekuwa akiwakilisha jimbo la Ndanda kupitia CHADEMA kutangaza kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM lakini bado anaendelea kupata stahiki zote kama mbunge na Ndugai bado anamtambua kuwa Cecil Mwambe ni mbunge wa Bunge la Jamhuri.

Kitendo cha Mwambe kuhamia CCM kilimpotezea sifa ya kuendelea kuwa mbunge, Hili la leo Spika wa Bunge amedhihirisha udhaifu alionao. Spika ni dhaifu na Bunge la 11 ni Bunge dhaifu mno katika historia ya Tanzania.

Huko ni kusigina katiba.
 
Kweli bwana. Eti Ndugai anasema haitambui barua ya katibu mkuu wa Chadema. Mwambe si alihama chama kwa hiari na barua aliyoandika ndiyo inatumika kama kielelezo ambayo spika analetewa nakala na Mwambe mwenyewe? Hili lizee kweli ni zero!
Hivi sheria ya uchaguzi inasemaje endapo jimbo linakuwa wazi dakika za majeruhi?
 
Kutumia madaraka vibaya na kuvunja katiba ya nchi ,ili uwe mbunge lazima upate ridhaa ya chama cha siasa, Sasa yeye alipata ubunge kupitia chama cha siasa akajitoa kwenye chama kilichomdhamini ubunge kwa hiyo na ubunge wake unakoma
Pengine hajapokea barua rasmi toka kwa Mbunge na Chama cha Chadema anaanzia wapi kutamka sio mbunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, toleo la 2005, ibara ya 71 "Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo kati ya mambo yafuatayo." Kati ya hayo mambo ni kifungu kidogo cha (f) kinasema: "iwapo Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge"
 
Ujinga mzigo,Punguza mahabbah

Back
Top Bottom