Spika Ndugai ataka PAC kuwahoji watendaji wa Tanesco, TRC, Muhimbili na Posta kwanini hawakupeleka mahesabu kwa CAG!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
45,145
2,000
Spika wa bunge ameyashangaa mashirika makubwa nchini kama Tanesco, TRC, Muhimbili, MOI na Posta kushindwa kuwasilisha mahesabu yao kwa CAG.

Ndugai ameitaka kamati ya bunge ya mashirika ya umma PAC kuwaita watendaji wa mashirika hayo na ikiwezekana wataishauri serikali ivunje bodo za mashirika hayo.

Source ITV habari!
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,592
2,000
Hii PAC kisheria inatakiwa kuongozwa na wapinzani, hivi ni nani anaongoza hiyo kamati?

Na kwanini bunge huwa halipeleki mahesabu yao kwa CAG? namshangaa Ndugai anawasema hao wakati na yeye hana tofauti nao.
 

Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,919
2,000
Kwani reports za CAG zilicomment vipi kuhusu hayo Mashirika?
Kwanini wahusika wasipeleke mahesabu yao kwa CAG kwanza ili CAG awasilishe taarifa zao kwanza kwa Mh. Rais alafu ndio ziwasilishwe Bungeni?
Hata hivyo si vibaya kwa Mh. Spika kukumbushia mahesabu hayo ili ikiwezekana wahusika wafanyie kazi.
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
45,145
2,000
Hii PAC kisheria inatakiwa kuongozwa na wapinzani, hivi ni nani anaongoza hiyo kamati?

Na kwanini bunge huwa halipeleki mahesabu yao kwa CAG? namshangaa Ndugai anawasema hao wakati na yeye hana tofauti nao.
Inaongozwa na mama Kaboyoka wa Chadema!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom