Spika Ndugai asilaumiwe mpaka sasa

Hiv unadhn kayatamka bure?huyo hata akipelekewa taarifa pia anaweza kugoma kuwa hakuzipata,mwache adunde bhana kama kinga anayo nn kimtishe????hebu rejea maneno ya mkurugenzi kukanusha kupewa majina ya viti maalumu trh 20 kisha kubadili maneno yake kuwa alipewa majina trh 19.sasa hv kila kitu kinawezekana ili mfalme afurah.

Kufuatia matamshi ya Spika wa bunge leo bungeni wakati akiwaapisha wabunge wateule Humphrey Polepole na Bi. Riziki, ambapo Spika amewahakikisha ubunge wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wao na Chadema..
 
Kama kweli mbona NEC walikuwa wanajichanganya? Tarehe 20/11/2020 walisema hawajapokea majina (ukitaka ushahidi wa video nitakuwekea). Tarehe 27/11/2020 baada ya CHADEMA kusema majina ni fake wakaibuka wakisema walipokea majina tarehe 19/11/2020 kisha kamati ya NEC ikakaa tarehe 20/11/2020 kuchagua majina ya wabunge na madiwani kutoka kwenye majina waliopokea. Huu mbona ni mkanganyiko unaodhihirisha uongo mkubwa.
hapo ndio chadema walitakiwa kwenda NEC kuangalia hayo majina yalipelekwa na kusainiwa na kiongozi gani, kuna viongozi wamezungukana hapo kati ya mnyika na mbowe, na kupeleka majina NEC kinyemela
 
Sasa yeye ni kiziwi asiyesikia sekeseke hii yote iliyotokea???, anashindwa hata kuwasiliana na NEC???---- nchi gani hii imekosa coordination!!!. Hawa akina Ndugai na NEC wanalao jambo katika suala zima la huo Ubunge, wameisha likoroga kwenye uchaguzi bado wanendelea kulikoroga tena..
Inawezekana mnyika ameshirikiana na akina mdee kupeleka majina nec bila kushirikisha akina mbowe n.k. hayo majina yaliyopelekwa nec yachunguzwe yalisainiwa na nani.
 
Kufuatia matamshi ya Spika wa bunge leo bungeni wakati akiwaapisha wabunge wateule Humphrey Polepole na Bi. Riziki, ambapo Spika amewahakikisha ubunge wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wao na Chadema...
Kama hana taarifa mbona ameshawahukumu Mbowe na Mnyinga? Ndugai ni mgonjwa anachana naye
 
Kufuatia matamshi ya Spika wa bunge leo bungeni wakati akiwaapisha wabunge wateule Humphrey Polepole na Bi. Riziki, ambapo Spika amewahakikisha ubunge wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wao na Chadema...
UTARATIBU UWEPO AU USIWEPO HII NI VUTA NIKUVUTE YA ndugai na mzee meko , kuonyesha wakina mbowe nani anamamlakaa , wameishafukuzwa dunia inajua na hata wenyewe wanajua, wenye akili pia wamajua kwa tukio la kikao kile kuwafuta uanachama hawastahili kuwa wabunge, lkn kwa kuwa kuna watu hawatumii busara ktk kuiendesha hii nchi , yetu machoo
 
hapo ndio chadema walitakiwa kwenda NEC kuangalia hayo majina yalipelekwa na kusainiwa na kiongozi gani, kuna viongozi wamezungukana hapo kati ya mnyika na mbowe, na kupeleka majina NEC kinyemela
Mbona unaruka, waniini kauli za NEC zinajichanganya? Kwanini hilo hujibu? Maana kauli ya NEC ndiyo inajichanganya sasa kwanini kujichanganya huko ukuhusishe na Mbowe na Mnyika?
 
Mkuu, unaargue kama mtu layman kabisa asiyeelewa mambo. Sasa unataka speaker afanyie kazi habari za kusikia kutoka kwenye press conference? Chadema wasipopeleka barua rasmi ya taarifa maana yake ni kwamba hao wamama wataendelea kutambuliwa kuwa wabunge halali. Itakula kwa chadema!

Wewe ndiye layman khasa.

Wewe hujui kwamba NEC na Spika lao ni moja??, watendaji wa vyombo vya umma siyo "Robots" au computer wanaosubiri kuwa programmed, hao ni watu wanaotakiwa kuwa na fikra, utashi, na dhamira pia kutambua dhamana ya kutumikia umma, "Spika Mwenye busara na hekima na mwenye dhamira ya kutumikia umma" kamwe hawezi kushindwa kitatatua huo mgogoro,
kinachoonekana ni Spika naye ni sehemu ya huo mgogoro, ni mpishi wa huo mgogoro.

Hakuna asiyejua jinsi upinzani ulivyoumizwa katika uchaguzi na huo mgogoro ni muendelezo hayo maumivu tu.
 
inawezekana mnyika ameshirikiana na akina mdee kupeleka majina nec bila kushirikisha akina mbowe n.k. hayo majina yaliyopelekwa nec yachunguzwe yalisainiwa na nani.

Sasa ndio inatakiwa akina mdee waende kuonana na uongozi wa chama kubainisha jambo hilo.
 
Mbona unaruka, waniini kauli za NEC zinajichanganya? Kwanini hilo hujibu? Maana kauli ya NEC ndiyo inajichanganya sasa kwanini kujichanganya huko ukuhusishe na Mbowe na Mnyika?
NEC walishasema, katibu mkuu wa CHADEMA ndio amepeleka hayo majina ya wabunge, na kwenye press ya mbowe hakujibu hili zaidi ya kujitetea kwamba hana taarifa, huoni CHADEMA wanajichanganya? ivi inawezekanaje Salim Mwalimu asijue taarifa za mke wake Esther Matiko ? inawezekanaje kigogo wa twitter awe na taarifa za yanayoendelea ndani ya chadema lakini Mnyika asijue, tuwe wakweli, baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanahusika
 
Sasa ndio inatakiwa akina mdee waende kuonana na uongozi wa chama kubainisha jambo hilo.
kila kitu kiko wazi, NEC wamesema majina yamepelekwa na katibu mkuu, na Mbowe kwenye press yake hakukanusha, huoni kuna namna hapo?
 
NEC walishasema, katibu mkuu wa CHADEMA ndio amepeleka hayo majina ya wabunge, na kwenye press ya mbowe hakujibu hili zaidi ya kujitetea kwamba hana taarifa, huoni CHADEMA wanajichanganya? ivi inawezekanaje Salim Mwalimu asijue taarifa za mke wake Esther Matiko ? inawezekanaje kigogo wa twitter awe na taarifa za yanayoendelea ndani ya chadema lakini Mnyika asijue, tuwe wakweli, baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanahusika
Hizo ni assumption zako. Lakini NEC wao wenyewe wamejichanganya kauli zao zinajichanganya hata wewe umeshindwa kueleza ni kwanini wametoa kauli mbili tofauti, na video ikawaumbua. Umeshindwa kueleza na wao NEC kwasababu wamehusika katika mchezo mchafu hawana maelezo, Narudia tena tarehe 20/11/2020 NEC walisema hawajapokea majina kutoka CHADEMA.

Tarehe 27/11/2020 NEC hao hao wakasema walipokea majina tarehe 19/11/2020 (siku moja kabla ya siku walituambia kuwa hawajapokea majina) halafu wakaendelea kwa kutuambia kamati ya NEC ikakaa tarehe 20/11/2020 (Siku ambayo ndipo walitutangazia kuwa walikuwa hawajapokea majina) wakakaa kuchagua wabunge na madiwani kutoka kwenye majina waliopokea.

Ni kituko kama si ajabu ni mtu wa ajabu ambaye anaweza fumba macho asione mkanganyiko huu. Ila uzuri teknlojia imewaumbua kama kusingekuwa na video wangekana kauli zao ila basi tu wametoa tamko walipogundua mkanganyiko wakaamua kukaa kimya.
 
Write your reply...
Kuzunguka kote kumfuatilia SPIKA ni kupoteza muda, Chadema waiandikie NEC juu ya hatua ya kuwavua uanachama. Hivyo kungojea NEC ipeleke taarifa kwa SPIKA, Nasikia walipewa siku 30 za kujitetea kama baada ya hapo hawajafanya hivyo CHADEMA ipigilie msumari maamuzi yake, Waliitwa wakakataa, sasa nafasi nyingine wamepewa.
 
Hivi wewe unawaza kisawa sawa kweli?.Ndugai mbona amewahi kuwafukuza akina Halima Mdee na Ester Bulaya bungeni Mara kadhaa,hapo hakuwanyanyasa?,Ccm mmewahi kumfukuza Sofia Simba na wenzake,Mliona chadema inasema kitu?,CCM mliwapiga na kuwajeruhi hao alina Mdee mbona tulinyamaza?.Usiwe punguani.

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
Wewe ndio akili hazipo sawa. Hao kina Mdee na Bulaya walisimamishwa kwa mujibu wa kanuni za bunge.
 
Back
Top Bottom