Spika Ndugai asema Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mahakama pekee wanaweza kumuambia kuwaondoa Bungeni Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,426
7,737
Leo jijini Dodoma wameapishwa wabunge wapya wawili walioteuliwa na Rais Magufuli kwenye nafasi zake za wabunge walioteuliwa na Rais, miongoni mwa waliohutubu kwenye hadhara hiyo ni naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dkt. Tulia Ackson ambaye ameelezea umuhimu wa Bunge kuwa karibu na serikali.

Mwingine aliehutubu ni Spika wa Bunge, Job Ndugai ambae ameendelea kuelezea sakata la wabunge 19.

==========

TULIA ACKSON: Huwa si kazi rahisi sana mtu kujisemea mwenyewe mheshimiwa spika, dakika chache nilizopewa kusalimu, nichukue fursa hii kukupongeza sana kwa kazi unayoifanya.

Haijalishi watu wangapi watu wangapi hawataona lakini wako watanzania wanayoiona kazi nzuri unayoifanya.

Nasema hivi nitoe mifano kidogo, ushirikiano kati ya Bunge na serikali ni wa muhimu na wapo watu hufikiri Bunge likiwa karibu sana na serikali au likishirikiana kwa karibu sana na serikali basi bunge ni dhaifu. Watu huanza kusema maneno mengi lakini mheshimiwa Spika nichukue fursa hii kwa niaba ya watanzania wazalendo wanaoielewa kazi yako kukupongeza kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya.

Katika nchi hii katika miaka mitano iliyopita yamefanyika mabadiliko makubwa ambayo kila mwananchi anayependa kuona maendeleo ameyaona. Yamefanyika mabadiliko mengi katika katika sheria za uvuvi na sasa tukizungumza kuhusu uvuvi unavyolisaidia Taifa hili hautasahaulika kutaja mheshimiwa spika kwa sababu wewe ndie ulieunda kamati zikafanya kazi na mabadiliko yakafanywa na Bunge.

SPIKA JOB NDUGAI: Nichukue pia nafasi hii kuwwambia watanzania kwa baadhi ya mambo yanayoendelea tuendelee tu kuwa wavumilivu, tuangalie hiyo sinema ambayo haijawahi kutokea kwenye yoyote ile duniani kwamba spika unaambiwa uwafukuze wabunge 19 wanawake.

Alafu unauliza kosa lao nini? Unaambiwa kosa lao ni kwasababu waliitikia wito wako wa kuja kuapishwa kwako alafu na wewe ukawaapisha. Hivi duniani kote mliwahi kuona wappi kitu kama hicho? Kwa sababu kwa njia ya wale na wengine wanaofanana nao kwa maana ya viti maalum, ruti yao kwa spika ina ruti mbili.

Njia moja ni tume ya uchaguzi kuniandikia na kusema hawa wanastahili kuwa wabunge, mheshimiwa Spika waapishe na huo ndio utaratibu na utaratibu huo ulifuatwa nikawaapisha.

Upande wa pili ni kwamba majina ya wanaoapishwa hapa kwa njia hiyo huwa yanakuwa yamepita kwa kutangazwa kwenye gazeti la serikali. Gazeti la serikali lilikwisha watangaza kwa kuwaorodhesha kwa majina mmoja mmoja katika hao 19, kwakua hayo yametekelezwa ipasavyo na spika nae kawaapisha alafu mtu mwingine anasema kosa la hao ni wewe kuwaita na kuwaapisha kwa hiyo wafukuze, hivi na mimi si nitaingie kwenye Guiness book spika wa ajabu kabisa ambae hajawahi kutokea dunia kuwafukuza wabunge kwa kosa la kuwaapisha.

Ufutiliaji wa Jambo hili kama lina walakini mahali sio kwa spika, nalo lina ruti mbili au zaidi. Ruti moja kufuatilia tume ya Taifa ya uchaguzi kwa sababu wao ndio wanafatilia mambo ya uchaguzi na kuniletea majina, kwa hiyo majina yote niliyoletewa na tume tumeshayafanyia kazi na kwa upande huo hakuna shida.

Ruti ya pili kama jamaa zetu wamesahau ni mahakamani, mahakama ndio inaweza kuniambia kuna walakini kwa mbunge A, B, C kwa hiyo chukua hatua hii kwa kosa hilo.
 
5678901.jpg
 
Spika Ndugai amesema aliwaapisha wabunge 19 wa CHADEMA baada ya kupokea majina kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na pia kuyasoma majina hayo katika Gazeti la Serikali.

Ndugai amesema kama kuna tatizo lolote kuhusu hawa Wabunge wa CHADEMA basi ama wakaulizwe Tume ya Uchaguzi au CHADEMA waende kulalamika Mahakamani kwani yeye kama Spika hausiki kwa sababu majina aliletewa kwa mujibu wa Katiba na Sheria.

Source: Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!
 
Wakati Wa Nyani Kumkana Mwanaye
Siku Ya Kufa Nyani Miti Yote Huteleza
😁😂😅😄😃😀😁🤣
 
Umefika wakati sasa hivi hamna kungojea tena nchi yetu kuongozwa na mwanamke. Mungu tuokoe watu wako.

Wanawake waheshimiwe
 
Ushauri waheshimiwa wabunge na viongozi wa bunge chapeni kazi achaneni na kelele za vijana wa bavicha, kazi hii mtuachie sisi tunaoona utendaji uliotukuka katika awamu hii ya 5.

#maendeleo hayana chama.
 
Kwa iyo wewe unaona wanavyofanya haya mambo ni sahihi? Kwanini mnapenda kuchezechezea mustakabali wa taifa na maisha ya Watanzania? Hamuoni kabisa aibu mnavyoliangamiza taifa? Mnaishi kimzahamzaha tu. Kisa mmebahatika kushika madaraka.
Mkuu kina Mdee kutumia haki yao ya kikatiba kwenda kuapa kuwa wabunge kulingana na asilimia walizopata kwenye uchaguzi mkuu ni kuangamiza taifa?
 
Kwa iyo wewe unaona wanavyofanya haya mambo ni sahihi? Kwanini mnapenda kuchezechezea mustakabali wa taifa na maisha ya Watanzania? Hamuoni kabisa aibu mnavyoliangamiza taifa? Mnaishi kimzahamzaha tu. Kisa mmebahatika kushika madaraka.
Wanaotesha mizizi ya kitapeli tapeli kila mwanafunzi sasa hivi ana amini katika utapeli utapeli kama serikali inavyofanya haamini tena kuna mahakama na haki wana amini udanganyifu ndio uzalendo na sheria wala katiba sio ya kuheshimu ni mbwembwe tu!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom