Spika Ndugai asema Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mahakama pekee wanaweza kumuambia kuwaondoa Bungeni Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

CHADEMA leo wamesema wanaenda mahakamani.

Spika leo kawaambia CHADEMA waende mahakamani.

Sasa nimeanza kuwaelewa!
 
Ushauri waheshimiwa wabunge na viongozi wa bunge chapeni kazi achaneni na kelele za vijana wa bavicha, kazi hii mtuachie sisi tunaoona utendaji uliotukuka katika awamu hii ya 5

#maendeleo hayana chama
Unamaanisha hata baba Msekwa pia alikua hajitambui kusema kisheria hawana haki ya kuwa wabunge?
 
Mambo ya aibu!Katiba inasema kuwa chama cha siasa kikishamvua uanachama mbunge basi speaker anatakiwa kumfutia ubunge mbunge huyo ila yeye anang'ang'ania hadi apokee amri kutoka NEC au mahakamani,yaani anatembea na katiba yake mfukoni!

10201208.jpg
 
Hivi kwanini Ndugai anaweweseka? Kama anawahitaji aendelee nao tu , Chadema ishawavua uanachama , na Katiba ya Tanzania inawataka wabunge wawe wanachama wa chama cha siasa .
 
Spika Ndugai amesema aliwaapisha wabunge 19 wa CHADEMA baada ya kupokea majina kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na pia kuyasoma majina hayo katika Gazeti la Serikali...
Kikwetu tunasema ingoma inogilee.
Mi naomba niulize swali kwani Alie peleka majina ya hawa wabunge 19 NEC bado chadema hawajampata?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kwani alivyomrudisha Mwambe bungeni si alishaingia kwenye Guiness Book of World Records, au hajui hilo? Kweli ana faili Mirembe.
 
Hivi kwanini Ndugai anaweweseka ? Kama anawahitaji aendelee nao tu , Chadema ishawavua uanachama , na Katiba ya Tanzania inawataka wabunge wawe wanachama wa chama cha siasa .
Keshajua kachemsha, kwa hiyo mikelele anajitahidi kutafuta kuungwa mkono na li Jiwe.

Betina nae anazidi kuwa kichekesho, kwa kutaka kufisha uharamia uliyofanyika.

Iwe mvua au jua, hakuna kurudi nyuma kwenye swala hili.
 
Maswali mepesi tu nimuulize Spika Ndugai

Je, wakati akina Sophia Simba wanafujuzwa Uanachama wao CCM, si aliwafukuza moja kwa moja, bila kwanza kungojea maamuzi ya mahakama?

Je walipofukuzwa uanachama wao wale wabunge wa viti maalum wa CUF, nao si aliwafukuza moja kwa moja, bila kusubiri maamuzi ya mahakama?

Kwanini kuwe na uamuzi tofauti safari hii walipofukuzwa uanachama wabunge wa viti maalum wa Chadema?

Ni kwanini yeye Spika anakidhalilisha kiti chake cha Uspika na anafanya "double standard" kiasi hicho katika kiti hicho cha U-Spika?
 
Back
Top Bottom