Spika Ndugai asema huenda Lema ana msongo wa mawazo kwani ana deni la Tsh. Milioni 644! Amtaka afike kwenye Kamati ya Maadili leo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Spika Job Ndugai ameagiza Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA), afike mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge leo saa 8:00 mchana kujibu tuhuma zinazomkabili za kulidharau na kulidhalilisha Bunge

Spika amesema kuwa hilo si dhaifu na yeyote atayeingia kwenye 18 zao anaalikwa kwenye mchezo huo

Aidha, amema kuwa huwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini ana msongo wa mawazo kwani tangu aingie Bungeni, amekopa Tsh. Milioni 644/-

Katika hatua nyingine amemfukuza ndani ya Ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko(CHADEMA) baada ya kupiga kelele kumpinga kiongozi huyo kutaja deni la Lema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliona walivyokuja na matoleo tofauti tofauti ya kamusi na dictionary kisa wanatafuta kifungu cha kuitwa dhaifu. Kwa weledi, msukumo na nguvu ile ile, anaweza kueleza anapata wapi madaraka na uhalali wa kutaja deni la mtu binafsi hadharani? Kwa sheria ipi?
 
Back
Top Bottom