Spika Ndugai anaendesha Bunge kwa matakwa yake binafsi na si kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kuandika katiba mpya hakuna maana kama hii iliyopo haifuatwi, siku Chama cha Mapinduzi kikiondoka madarakani mheshimiwa Ndugai anastahili sio tu kushtakiwa, bali kunyang'anywa stahili za uspika anazofaidi kwa kutumia kodi za wananchi, pamoja na yeye wafuatao nao watakuwa pamoja nae mahakamani kwa kushindwa kusimamia kiapo Chao :
1. Waziri wa katiba na Sheria
2. Mwanasheria mkuu wa Serikali

Mheshimiwa Speaker hastahili kuendelea kuhudumiwa na walipa kodi masikini wa Tanzania
IMG_20200512_064151.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuandika katiba mpya hakuna maana kama hii iliyopo haifuatwi, siku Chama cha Mapinduzi kikiondoka madarakani mheshimiwa Ndugai anastahili sio tu kushtakiwa, bali kunyang'anywa stahili za uspika anazofaidi kwa kutumia kodi za wananchi, pamoja na yeye wafuatao nao watakuwa pamoja nae mahakamani kwa kushindwa kusimamia kiapo Chao :
1. Waziri wa katiba na Sheria
2. Mwanasheria mkuu wa Serikali

Mheshimiwa Speaker hastahili kuendelea kuhudumiwa na walipa kodi masikini wa Tanzania View attachment 1447567

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo Spika anashangaza kwa kuwa jambo kama hilo linapokuwa limeamriwa na Chama chake cha Mapinduzi anatekeleza Mara moja.........

Lakini inapotokea uamuzi umefanywa na chama cha Chadema, hataki kuutekeleza!
 
Am speechless
Huwezi mvua uanachama mbunge kwa kutekeleza majukumu yake ya kibunge bungeni

Kazi ya mbunge ni.kuhudhuria vikao vya bunge sasa Wewe ujlkisema unamfukuza kakosea kuhudhuria vikao vya bunge akili unakuwa huna .Nasimama na spika yuko sahihi mbunge kuhudhuria vikao vya bunge sio kosa .Hakuna awezaye mwadhibu kuwa eti kakosea kuhudhuria vikao vya bunge !!!
 
Nimestushwa sana na kauli ya Spika wa Bunge la Tanzania, aliyoitoa jana kuhusiana na wabunge wa Chadema, waliofukuzwa uanachama katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema.

Spika Ndugai amenukuliwa akiwaambia wabunge hao kuwa hatambui kufukuzwa kwao uanachama na chama chao cha Chadema na hivyo waendelee na vikao hivyo vya Bunge, kwa kuwa yeye ndiye aliyewaapisha kuingia Bungeni humo na hivyo hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kuwavua ubunge wao.

Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 71(1)(el) inatamka hivi "Mbunge atakoma kuwa mbunge ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge" mwisho wa kunukuu

Huyu Spika Ndugai anasahau kuwa hata yeye kabla hajakabidhiwa mamlaka aliyo nayo aliapa kuitii na kuiheshimu Katiba hiyo ya nchi

Sasa nimuulize Spika Ndugai, hicho kiburi cha kuwaambia wabunge hao waliovuliwa uanachama wa chama chao, waendelee na ubunge wao anakipata wapi?

Katiba ya nchi ipo wazi kabisa kuwa mtu anaendelea kuwa Mbunge pale tu anapoendelea kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

Hivi hawa akina Silinde, hivi sasa wameshafukuzwa uanachama wa chama cha Chadema, kilichowapa ubunge huo, sasa yeye Spika Ndugai anapowaambia waendelee na ubunge wao, wanakuwa wabunge wa chama kipi cha siasa?

Kwa kuwa kwa kufukuzwa uanachama wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba ya nchi "automatically" wamepoteza pia ubunge wao.

Kama Spika Ndugai anawaambia hao wabunge waendelee na ubunge wao, wanakuwa ni wabunge wa Spika Ndugai na wala siyo wabunge wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo yeye Spika Ndugai aliapa kuitii na kuiheshimu kabla hajakabidhiwa madaraka hayo aliyo nayo hivi sasa.
₩Mgogoro huu bado mbichi sana. Hapo kuna hoja ya haki ya kimsingi waliyonayo na kauli za mh spika. Pia tuelewe kuwa muda wa bunge maisha. Over
 
spika hajui thamani ya kiti alichokalia. anaona kama hisani aliyopewa na magufuli. yale matibabu ya bilioni na ushee yanamtesa. asipofuata maelekezo anazitapika hizo hela
 
Huyu Spika Ndugai nilimshangaa pia alipotamka kuwa Mbunge Mbowe hatarudi kwenye ubunge wake, hapo mwisho wa mwaka baada ya uchaguzi mkuu.

Hivi yeye kama Spika anawezaje kutoa matamshi kama hayo wakati yeye siyo mmoja wa wapiga kura wa jimbo la Hai, analotoka Mheshimiwa Mbowe?
Amejisahau katoa siri, ina maana wanayo list ya wabunge wa CDM ambao watafanya kila wawezavyo wasirudi bungeni. Mbowe naye yumo kwenye hiyo list yao, ndiyo maana kajisahau karopoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofauti ni kwamba mbowe avunji Katina ya chamhuri tofauti na ndugai
Mbowe ndie kavuja katiba .Kaxi ya mbunge ni kuhudhuria vikao vya bunge huwezi mwandikia mbunge barua kuwa kakosea kuhudhuria vikao vya bunge hivyo afukuzwe uanachama!!!!!
 
Kuandika katiba mpya hakuna maana kama hii iliyopo haifuatwi, siku Chama cha Mapinduzi kikiondoka madarakani mheshimiwa Ndugai anastahili sio tu kushtakiwa, bali kunyang'anywa stahili za uspika anazofaidi kwa kutumia kodi za wananchi, pamoja na yeye wafuatao nao watakuwa pamoja nae mahakamani kwa kushindwa kusimamia kiapo Chao :
1. Waziri wa katiba na Sheria
2. Mwanasheria mkuu wa Serikali

Mheshimiwa Speaker hastahili kuendelea kuhudumiwa na walipa kodi masikini wa Tanzania View attachment 1447567

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa unachanganya mambo Nyalandu kosa alilofukuzwa na chama sio kuhudhuria vikao vya bunge Uanachama wake ulikoma kwa sababu zingine sio za ubunge wake au kuhudhuria bungeni.Vyama ruksa kuadhibu uanachama wao lakini sio kuadhibu MTU kwa kuhudhuria vikao vya bunge wakati unajua ni wajibu wake hilo hakuna

Usilinganishe ya Nyalandu na hilo wakilofanya chadema

Chadema wanaadhibu mbunge kwa kuhudhuria vikao vya bunge hiyo no haikubaliki popote
 
Back
Top Bottom